Alisema kuwa anatambua kuwa kuna baadhi ya watu wameumia baada ya ushindi huo, lakini hilo halimkatishi tamaa na badala yake kilichobaki ni kazi moja tu na kuhakikisha analinda heshima ushindi huo.
"Wasionitakiwa mema ninawasamehe kwa sababu hawajui watendalo, lakini wanaojua kile ninachokifanya wanajali kazi zangu na wananitakia mema, ila hao wanaonishambulia kwenye mitandao ya kijamii waendelee," alisema Lulu.
Lulu aliliambia gazeti hili kuwa tangu atwae tuzo hiyo amezushiwa mambo mengi ambayo hayana ukweli.
Msani huyo alisema kuwa alianza kujihusisha na sanaa akiwa na umri wa miaka mitano na ameendelea hadi sasa, lakini ameshangaa kusemwa kuwa ushindi wake ushindi wa tuzo yake umetokana na ushirikiana.










