Kwa kutambua hilo msanii wa muziki wa kizazi kipya Snura Mushi amesema huwa anakuwa makini kwa kuchukua khanga katika mkoba wake kila anapotoka kwenda kwenye safari mbali na kwake.
Iwapo umewahi kujiuliza kwanini kimwana huyo hutembea na mkoba mkubwa kila mara, basi mwenye anasema kuwa huweka vitu vya muhimu ikiwamo khanga kwa ajili ya dharura, kwa vile anatambua kuwa yeye ni mwanamke aliyefundwa.
Msanii huyo aliiambia Nipashe kuwa amefundwa na atatambua umuhimu wa mavazi kwa kuzingatia maadili ya mwanamke wa Kiafrika ndio maana siku zote hawezi kutembea bila kuwa na mkobwa mkubwa.
Kwa ujumla ni kwamba katika mkoba wangu huwa ninaweka vitu vingi zikiwamo khanga mbili kwani bila hizo siwezi kabisa kutembea kwa uh uhuru kwani ninatambua umuhimu wa mavazi," alisema Snura.
Alisema kuwa anawashangaa baadhi ya wanawake wenzake ambao huwa hawapendelei kubeba vitu kama hivyo kwa makusudi ama kwa kutotambua umuhimu wake na kuwataka wawe wanakumbuka kubeba khnga katika mikoba yao.










