Alisema kuwa jitihada zao za kumuharibia taswira yake kwenye jamii zimegonga mwamba na kufafanua kuwa hana tabia ya kujirusha sana na vimwana zaidi ya kufanya kazi ya muziki.
"Maisha yangu yako kwenye serikali yangu, watu wasitake niishi wanavyotaka wao...wanajaribu sana kuchafua jina langu kwa mashabiki zangu, na pia wanajarbu kushusha heshima yangu kwa wanaonieshimu ila wamechelewa sana," alisema Baraka.
Akizungumza na Nipashe alisema kuwa mashabiki wake hawawezi kumchukia kwa sababu tu ya uvumi na uzushi unaoendelea na kwamba ameshawajua anayewatuma watu kumchafua kwa kumzushia mambo ya mahusiano ya mapenzi na watu mbalimbali.
Mara kwa mara Baraka amekuwa akisema kuwa hataki kujihusisha na skendo ili kulinda heshima yake na kuweka wazi kuwa anachozingatia ni kazi zake ili aweze kuwa msanii wa kimatifa.










