Nature: Ukileta pozi unapotea

04May 2016
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Lete Raha
Nature: Ukileta pozi unapotea

MSANII ambaye amedumu kwenye gemu kwa muda mrefu, Juma Nature, amesema kuwa siri ya kuendelea kutamba hadi sasa inatokana na kuheshimu mashabiki wake.

Juma Nature.

Alisema wapo baadhi ya wasanii ambao wamepotea kabisa baada kupata umaarufu kidogo tu na kisha kuanza kuringia mashabiki na kusahau kuwa wao ndiyo waliowafikisha hapo walipo.

"Siyo vizuri kuwaringia watu waliokuweka mjini, ukitaka wakupoteze, wewe waringie tu. Pita mitaani na kunyanyua mabega juu bila kusalimia watu, utakiona cha moto," amesema Nature.

Bila kuwataja majina, Nature alisema kuwa wapo ambao wamepotezwa na mashabiki wao na sasa hawana hamu na muziki wa kizazi kipya walioutegemea, kwa sababu tu ya kutotambua umuhimu wa mashabiki.