Dawa za kulevya zamuumiza Janjaro

04May 2016
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Lete Raha
Dawa za kulevya zamuumiza Janjaro

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Dogo Janja a.k.a Janjaro, amesema anaumia anapoona baadhi ya vijana wanajihusisha na matumizi ya dawa za kulevya na kuiomba serikali kuwakamata wauzaji wa dawa hizo, kwa madai kwamba wanajulikana.

Dogo Janja a.k.a Janjaro.

Alisema mtaani kwake Ngarenaro, Arusha alikotokea kuna wadogo zake, kaka zake na baadhi ya ndugu zake, ambao hataki hata kufikiria itakuwaje akisikia mmoja wao ameingia katika janga hilo, hivyo ni muhimu wauzaji wakamatwe mapema iwezekanavyo.

"Mimi ninahitaji sapoti ya mtaa kuongea na vijana wenzangu, unajua wengi ambao wamejikita humo ni wadogo zangu, kaka zangu na baadhi pia ni ndugu zangu... inaniuma kwani wanaouza dawa hizo wanajulikana, wakamatwe," amesema Janjaro.

Dogo Janja amesema hayo alipokuwa akizungumza na mashabiki wake kwenye mtandao wa kijamii akieleza kuwa muziki umemfikisha mbali kutoka kuwa mpiga debe mpaka mpigiwa debe.