Mwanaheri ana deni kwa mashabiki

29Feb 2016
Sabato Kasika
Nipashe
Mwanaheri ana deni kwa mashabiki

KWA kawaida mtu anapopata mafanikio katika shughuli zake huwa sio vibaya kukumbuka na kuwashukuru wale ambao kwa namna moja ama nyingine wamechangia mafanikio hayo.

Mwigizaji wa filamu,Mwanaheri Afcely

Mtayarishaji na mwigizaji wa filamu nchini, Mwanaheri Afcely ni miongoni mwa wanatambua na kuthamini mchango wa mashabiki wake.

Msanii huyo amesema kuwa ana deni kwa mashabiki wake na lazima alilipe kwa wakati muafaka.

Mwanaheri alisema amefika hapo alipo kutokana na kuungwa mkono na mashabiki pamoja na wasanii wenzake.