Barbie, ambayo inaongoza duniani kwa kuingiza mapato ya dola bilioni 1.2, ilianza kuonyeshwa nchini Algeria Julai 19, 2023 kabla ya kuondolewa kwenye ratiba zao siku ya Jumapili bila maelezo."Algeria imeingia katika malumbano kuhusu Barbie kutokana na sinema hiyo kuonyesha matukio yaliyokusudiwa kwa hadhira ya watu wazima na dokezo la ushoga.” tovuti ya habari ya TSA iliripoti.
"iliondolewa kwa kutumia uangalifu na busara", Ingawa sinema hiyo ilitarajiwa sana na jumuiya za LGBTQ duniani kote, filamu haionyeshi waziwazi mahusiano ya jinsia moja au mandhari ya ajabu” tovuti ya habari ya TSA iliripoti.









