BOOMPLAY, Itel zazindua kampeni ya utambulisho wa simu za p55 series

29Jan 2024
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
BOOMPLAY, Itel zazindua kampeni ya utambulisho wa simu za p55 series
  • Utambulisho huo utafanyika vyuoni ukiambatana na Tamasha la Muziki

Katika kuanza mwaka kwa njia ya kusisimua na katika harakati za kuonyesha ushirikiano baina ya teknolojia na muziki, App ya muziki inayoongoza barani Afrika, Boomplay na chapa ya Itel, ...

..wameungana kuzindua Kampeni ya utambulisho wa simu za Itel P55 vyuoni ikiambatana na Tamasha la muziki kwa vyuo vikuu vilivyochaguliwa kote barani Afrika. 

 

Kampeni hiyo iliyopewa jina la "Power Up Your Life", inajumuisha matukio mbalimbali ya kuonesha bidhaa na tamasha kubwa la muziki ambapo chapa hizi mbili zitagusa maisha ya wanafunzi na umma kwa ujumla ili kuonyesha bidhaa mpya kutoka Itel lakini pia kuwapa fursa ya kufaidi idadi kubwa ya muziki kupitia App ya Boomplay.

 

Kwa Tanzania, tukio hili la Boomplay na itel P55 Series limepangwa kuanza rasmi kuanzia leo Jumatatu, Januari 29, 2024 hadi Jumamosi, Februari 3, 2024, kupitia vyuo vikuu viwili, Chuo Kikuu cha Dar es Salam (UDSM) na Chuo Kikuu cha Ardhi ambavyo kwa ujumla kutakua na maonesho mbalimbali ya bidhaa. Tamasha kubwa la muziki litakalokuwa na wasanii pendwa wa Tanzania akiweomo:- Barnaba, Meja Kunta, Kontawa, Platform, Lony Bway, Lody Music na wengine wengi litafanyika siku ya kilele katika Chuo Kikuu cha Dar es Salam (UDSM)-Mabibo Hostel.

 

Uzinduzi wa Simu mpya za itel P55 Series na E1 Smartwatch itakuwa ni kipengele maalum wakati wa mfululizo wa matukio yanayoendelea kwenye vyuo hivi, itel P55+, simu ya kwanza yenye wati 45 yenye uwezo wa kuchaji kwa haraka ina betri inayodumu muda mrefu na yenye burudani ya hali ya juu, ambayo inapendekezwa sana kwa wanafunzi na wapenzi wa muziki.

Akizungumzia ushirikiano huo, Natasha Stambuli, Meneja Mkuu wa Boomplay Tanzania alisema, "Tunafurahi kushirikiana na itel kuleta teknolojia bora na uzoefu wa burudani ya muziki kwa jamii ya wanafunzi nchini Tanzania. Ushirikiano huu unaenda sambamba na juhudi zetu za kupanua wigo wa usikilizaji wa muziki usio na kifani kwenye kupitia App yetu kwa watumiaji wetu na jamii inayowazunguka. 

 

Tunaamini kwamba tunaposhirikiana na wanafunzi na umma kwa ujumla, tunafungua njia zaidi kwa chapa ya Boomplay kupata uzoefu. Uzoefu huu wa muziki kutoka Boomplay ukichanganywa na teknolojia ya gharama nafuu na ya ubunifu kutoka itel ili kuleta kilicho bora kwa wanafunzi, unafanya ushirikiano huu kuwa wa kipekee kwenye suala zima la maendeleo ya kiteknolojia na burudani barani Afrika.

 

Kwa upande wa itel, Sophia Almeida, Meneja Uhusiano wa Umma wa itel Tanzania, alisema kwamba, “Itel inafurahia kushirikiana na Boomplay katika kuimarisha maisha ya wanafunzi kote Afrika. Dhamira yetu ya kutoa teknolojia ya gharama nafuu na ubunifu inaambatana kikamilifu na ujumbe wa Boomplay wa kutoa uzoefu wa burudani ya muziki. Pamoja, tunaleta muziki na mwanga wa teknolojia kwenye vyuo vikuu, na kuunda kumbukumbu isiyofutika ya burudani na uvumbuzi barani Afrika.

Boomplay inatambuliwa kama App inayoongoza barani Afrika kwa kusikiliza na kupakua muziki na inajivunia orodha kubwa ya idadi ya nyimbo za ndani na za kimataifa. Jukwaa hilo limekuwa sehemu muhimu la muziki kidijitali barani Afrika, ikiwapa watumiaji uzoefu wa kusisimua na wa kufurahisha kwa watumiaji wa bila malipo na wale wa bila malipo.

 

itel, Kampuni ambayo inayojulikana sana kutokana na kuwa na vifaa vya simu vya bei nafuu na ubunifu, imejenga uwepo mkubwa barani Afrika na kuwa chapa janja kimaisha kwa vijana wenye ujuzi wa teknolojia. Kujitolea kwake kutoa teknolojia ya hali ya juu kwa bei nafuu imewezesha kupata msingi mkubwa wa watumiaji kati ya wanafunzi na wafanyakazi vijana.

 

Wakati treni ya Boomplay na itel ⁇ Power Up Your Life ⁇ ikihamia vyuo vikuu, ushirikiano huo unatarajiwa kuacha alama ya kukumbukwa. Inaahidi uzoefu wa kushangaza wa teknolojia na burudani ya hali ya juu kwa wanafunzi, michezo ya kufurahisha, maonyesho ya muziki, maonyesho ya bidhaa za hivi karibuni kutoka itel na toleo la simu mpya ya itel P55 Series na E1 Smartwatch na zawadi kadha wa kadha. Jiunge na treni hii na kaa mkao wa kula wakati ambapo Boomplay na itel watakapokuletea burudani ya aina yake vyuoni.