Serikali yaitaka CMA kutatua Migogoro kwa haki

04Jan 2024
Ashton Balaigwa
MOROGORO
Nipashe
Serikali yaitaka CMA kutatua Migogoro kwa haki

SERIKALI imeionya Tume ya Usuluhushi na Uamuzi (CMA) kuhakikisha inafanya utatuzi wa migogoro mahali pa kazi kwa haki na wakati ili kuvutia wawekezaji waweze kusaidia kukuza uchumi wa Taifa.

Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako (katikati) akizungumza katika ufunguzi wa kikao kazi cha Tume ya Usuluhushi na Uamuzi (CMA) kilichofanyika mjini Morogoro. wengine ni viongozi mbalimbali wa CMA. Picha: Ashton Balaigwa

Imesema CMA ni lazima ijitengenezee mazingira ya kuaminiwa na wananchi,wafanya kazi,waajili na wawekezaji kwa kutenda haki ambayo itaonekana kwa pande zote mbili .

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako amesema hayo wakati akifungua kikao kazi cha CMA chenye lengo la kufanya Tathimini ya Utendaji wa kazi na mafunzo yanafanyika mjini Morogoro.

Amesema CMA inapaswa kutenda haki hizo ili kuweza kupunguza kesi zinazopelekwa juu kwa Majaji kutokana na baadhi ya wateja wao kukosa imani.

“Sasa wakati umefika kama CMA chombo ambacho kimeanzishwa kwa mujibu wa sheria tumpungeze kesi zinazopelekwa kwa Jaji sio tutoe haki tu lakini lazima iyonekane haki imetendeka kwa pande zote mbili” anasema Waziri Profesa Ndalichako.

Anasema tume hiyo imeaminiwa na Serikali ili kuweza kuleta mchango mkubwa na kasi ya kuongeza kasi ya wawekezaji katika sekta binafsi hivyo iwapo itatenda haki baina ya pande mbili kati ya mwajiri na mwajiliwa uwekezaji utaongezeka hapa nchini.

Awali mkurugenzi wa CMA, Usekelage Mpulla amesema katika utatuzi wa migogro ya kikazi,tume hiyo katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2023/24 ilikuwa na migogoro 4579 ikiwa ya kikazi 1859 iliyovuka mwaka na migogoro 2720 iliyosajiliwa ngazi ya usuluhishi na uamuzi .

Amesema hadi kufikia robo ya pili ya 2023 jumla ya migogoro 2712 sawa na asilimia 59 ya migogoro ya kikazi ilivuka mwaka na iliyosajili mwaka 2023/24 ilitatuliwa.

Mkurugenzi huyo amezitaja sababu zinazoongoza migogoro ya kikazi zipo tisa ambazo masuala ya ubaguzi, kusimamishwa kazi, kujengewa mazingira ya kuacha kazi,madhira,mikataba kuvunjwa isivyo halali,kutolipwa mishahara au kulipwa chini ya kima cha chini,haki za kichama, maombi /Tafsiri /Sheria .

Naye Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Dk. Yose Mlyambina amesema Mahakama hiyo inayohudumia mikoa ya Dar es Salaam na Pwani iliitisha majarada jumla 350 kati ya hayo 313 yaliwasilishwa mahakama kwa wakati 37 hayakuwasilishwa.