-uchimbaji madini kwa tija.
Dk. Kiruswa amesema hayo Februari 18, 2023 alipotembelea eneo la machimbo ya chumvi la Chakulu wilayani Uvinza mkoani Kigoma ili kuzungumza na kikundi cha Kinyo Farmers and Salt Works na Kikundi cha Twikome Salt Kinyo Chakulu.
"Ninasisitiza kuondoa migogoro katika eneo hili ili kuchochea ongezeko la uzalishaji wa Chumvi hapa nchini ili wachimbaji wanufaike na rasilimali hii muhimu," amesisitiza Dk. Kiruswa.
Katika hatua nyingine, Dk Kiruswa amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Uvinza kwa Kushirikiana na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kigoma afanye kikao na Wamiliki wa leseni na Àrdhi siku ya Jumatatu tarehe 20/02/2023 kwa ajili ya kuandika makubaliano yaliyofanyika katika mkataba.
Aidha, ameiagiza Tume ya Madini kushirikiana na Taasisi ya Jiolijia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kutembelea maeneo ya leseni za vikundi vyote ili kubainisha maeneo ambayo yanaweza kuchimbwa visima vya kuzalishia Chumvi.










