Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida,Yagi Kiaratu, akikabidhi hundi za mikopo hiyo leo (Februari 17, 2023) kwa vikundi hivyo amewataka wanufaika kufanya biashara kwa nidhamu ili waweze kurejesha mikopo hiyo na hivyo kujenga uaminifu wa kukopesheka.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Jeshi Lupembe, amesema mikopo hiyo iliyotolewa ni sehemu ya asilimia 10 ya fedha za mapato ya ndani na kwamba Manispaa hiyo imekuwa ikitekeleza kwa dhati kwa kutenga asilimia 10 kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Afisa Maeñdeleo ya Jamii Manispaa ya Singida, Upendo Naftari, amesema kati ya Sh.Milioni 305 zilizotolewa kwa vikundi hivyo, Sh.milioni 181 ni fedha za marejesho ambazo zilitolewa kwa vikundi 42 na Sh.milioni 124 ni asilimia 10 ya fedha za mapato ya ndani.










