Sangu ameyasema hayo jijini hapa wakati akizungumza na Waandishi kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Bodi hiyo huku akisema l;engo la kujengwa kwa mifumo hiyo ni kuwa na utaratibu wa kuwa na maghala ya kuhifadhia chakula yenye viwango vinavyotakiwa.
Alisema,mfumo huo pia utapunguza gharama kwa wanunuzi kutafuta mazao na badala yake kila kitu kitakuwa kwenye mtandao na kumrahisishia mnunuzi na kupata mazao anayoyahitaji kwa urahisi.
Vile vile alisema mifumo hiyo pia itawezesha minada kufanyika kimtandao ambapo minadada mingi itafanyika kwa mara moja na wanunuiz watapata fursa ya kuchagua wapi wakanunue mazao yao.
Aidha alisema kuanzia mwaka mwaka huu watashirikia na Tantrade ili kutafuta wanunuzi ambapo wanunuiz wan je hawatalazimika kuja hapa nchini kuona mazao kwa macho.
“Kwa hiyo tumejipanga kimkakati kufanya nao kazi ili kuhakikisha wakulima wananufaika na kazi za kilimo wananzozifanya maana watakuwa na masoko ya uhakika pamoaj na wanunuzi wa uhakika kutoka ndani na nje ya nchi.”alisema Sangu
Sangu alitumia nafasi hiyo kueleza mafanikio ya Bodi hiyo huku akisema,mazao mengi ya kimkakati yamekuwa yakizalishwa kwa tija kutokana na bei za mazo hayo kuongezeka.
“Kabla ya kuanzishwa mfumo wa stakabadhi za ghala,mazao mengi hasa ya kimkakati yalikuwa yakiuzwa bei ndogo ambayo ilikuwa hamnufaishi mkulima na badala yake ilikuwa ikimkandamiza kutokana na kutumia gharama kubwa katika uzalishaji lakini hapati mauzo ya kutosha,
“Lakini baada ya kuanzishwa kwa mfumo huo wa stakabadhi ghalani,mazao hayo yamekuwa yakiuzwa kwa bei nzuri ambayo inamletea tija mkulima na hivyo mazao hayo yameongezeka kwa uzalishaji wake tofauti na awali.”
Ameyataja baadhi ya mazao hayo yaliyoongeza tija katika uzalishaji na mapato kwa wakulima na Taifa kwa ujumla kuwa ni pamoja na Kahawa,korosho,choroko,Kakao .
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Sangu,Bodi hiyo imekamilisha kutengeneza ghala mtandao ambapo mwezi huu litazinduliwa na kwamba leseni zitatolewa kielektroniki kwa waendesha magahala hayo.










