Kwa sasa kahawa nyingi husafirishwa kwa njia ya magendo kwenda kuuzwa nchini Uganda.
Akizungumza katika kikao cha Bodi ya Kahawa mkoa wa Kagera kilichowausisha viongozi wa serikali kutoka halmashauri nane zilizo ndani ya mkoa wa Kagera, pamoja na wadau wengine wa zao hilo juzi:
Meya wa Manispaa ya Bukoba, Chifu Kalumuna alisema haoni sababu ya serikali kuwaingilia wakulima wa kahawa katika uuzaji wa zao hilo.
"Pindi wakulima wanapovuna wasiwekewe masharti yoyote katika zao lao wenyewe," alisema Kalumuna kwani "ni haki ya mkulima mwenyewe kuchagua soko ambalo analihitaji kutokana na vyama vya ushirika ambavyo vinasimamia ununuzi wa zao hilo kutothamini mkulima na kutompa bei iliyo bora.
"Mtu shamba la kwake mwenywe, ardhi ya kwake yeye, kahawa anaipanda na kuivuna yeye, alafu anatokea kiongozi wa serikali na kumpangia wapi pa kuuzia kahawa yake!
"Hilo ni jambalo (ambalo) haliingii akilini kabisa na halikubaliki kwani linawanyanyasa wakulima wa zao hilo."
Mmoja wa wakulima wa zao hilo, Saimoni Katto kutoka wilayani Karagwe alisema bado kuna ugumu mkubwa wa kudhibiti kahawa kuuzwa kwa njia ya magendo.
Alisema wakulima wanauza kahawa yao kwa magendo kutokana na kutokuwepo soko zuri na vyama vya ushirika kutowalipa wakulima bei nzuri na kwa wakati.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Salum Kijuu alivitaka vyama vikuu vya ushirika mkoani humo kuunda vyama vya kuweka na kukopa SACCOS, ili kuwezesha wakulima kukopa na kuboresha zao hilo na pia kuwezesha wakulima hao kulipwa kwa wakati.
Aidha, Kijuu alipiga marufuku kahawa kuuzwa kwa magendo na kuahidi kuwachukulia hatua kali watendaji wa serikali watakaobainika kujihusisha katika njama hizo, ikiwa ni pamoja na kuwafukuza kazi.
Kahawa husafirishwa kwa wingi kwenda nchini Uganda kupitia njia za magendo katika mipaka ya Murongowilayani Karagwe na Mtukula wilayani Missenyi.










