Hoja hiyo iliibuliwa na baadhi ya wafanyabiashara katika kikao cha wawekezaji ikiwa ni siku ya tatu ndani ya maonesho ya wiki ya mwanakatavi ambayo ni siku ya uwekezaji na kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo ndani ya mkoa.
Akijibu hoja hiyo Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuph amewahakikishia kuwepo kwa usalama wa kutosha na kuahidi kuzifanyia kazi changamoto ndogo zinazojitokeza.
Mkoa wa Katavi bado unaendelea na maonesho ya wiki ya mwanakatavi amb+apo kabla ya kikao hicho Jamila alitembelea na kukagua mabanda mbalimbali yaliyopo katika viwanja vya azimio yanakofanyika maonesho hayo.










