Serikali yaona fursa lukuki uwekezaji viwanja vya ndege

29Oct 2023
Na Mwandishi Wetu
Dar es salaam
Nipashe Jumapili
Serikali yaona fursa lukuki uwekezaji viwanja vya ndege

KAMPUNI za Hunan Xi Yue Culture Media Co na Hunan Xi Yue International Tradind Co Limited zinazoongoza kwenye biashara ya maua nchini China zimemesema zipo tayari kushirikiana na sekta ya anga na wadau wengine kuwekeza nchini.

Uwekezaji huo ni katika mnyororo wa thamani wa uzalishaji,usindikaji maua nchini kwetu na kuyauza China

Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi,Profesa Godius Kahyarara,mara baada ya kufanya mazungumzo na wawakilishi wa kampuni hizo katika ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan kushiriki kongamano la biashara nchini Zambia.

"Tayari mazungumzo yameanza na nimeona ni fursa kubwa hasa jwa ndege zetu za mizigo na chanzo kikubwa cha fedha za kigeni,"amesema.

Kwa mujibu wa Profesa Kahyarara, kwa sasa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), lina ndege kubwa ya mizigo yenye uwezo wa kubeba tano 54, za abiria za masafa marefu yaani Dreamliner zipo mbili zenye uwezo wa kubeba tani 25 za mizigo.

Aidha,amesema Tanzania inauza nje kiasi kidogo cha maua chenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni moja,kiwango kinachozidi mapato yote ya bidhaa za kilimo kwa mwaka.

Amesema wizara imejipanga vyema kutumia maeneo yaliyotengwa mfano Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjara ambako kuna ardhi yenyebukubwa wa hekta 1,200 zinazofaa kwa uwekezaji huo.

"Wizara ya Uchunguzi itahamasisha wizara nyingine pamoja na halmashauri za wilaya na mikoa ya Kilimanjaro,Njombe,Mbeya,Arusha,Iringa,Manyara na Songwe kuchangamkia uwekezaji huo.