Baada ya kuibuka mshindi Christina alikabidhiwa jokofu la kisasa, Televisheni, music system ya kisasa pamoja kipashia Moto vyakula.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa zawadi hizi, Christina aliishukuru kampumi ya Tigo kwa kuendesha kampeni hiyo na kuwataka Wananchi wengine kuchangamkia fursa ya kushinda.
"Nimekuwa nikitumia mtandao wa Tigo, nafanya miamala kupitia tigopesa mara kwa mara, hii ndio sababu ya kushinda kwangu, yoyote anaweza kushinda", anasema Christina.
Kwa upande wake Meneja Mauzo wa Kampuni hiyo kanda ya Kinondoni Kaskazini, Shadrach Mutalemwa ambaye alimkabidhi mshindi zawadi zake, ameshauri wateja wa kampuni hiyo kufanya malipo mbalimbali kwa kutumia Tigopesa ili kujiweka katika nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali katika kampeni hiyo.










