100 wapewa mafunzo ya ujasiriamali na TWCC

18Jan 2024
Shaban Njia
KAHAMA
Nipashe
100 wapewa mafunzo ya ujasiriamali na TWCC

CHAMA cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC) kwa kushirikana na Trade Maker wameendesha mafunzo kwa wajasirimali kuhusu kanuni, taratibu na sheria za kufanya biashara kwenye Soko Huru la Afirika (AfCTA) kwa lengo la kuwainua kuwa wafanyabiashara wakubwa hapo baadae.

Aidha, wajasiriamali hao ni kutoka mkoani Shinyanga katika Halmashauri za Kishapu, Manispaa ya Shinyanga, Shinyanga Vijijini, Ushetu, Msalala pamoja na Manispaa ya Kahama na yataendeshwa kwa muda wa siku mbili wilayani kahama kuanzia hivi sasa na yataendeshwa na TBS, SIDO, Brela, TRA, TCCIA, GS1 na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa serikali.

 

Mkurugenziu wa chama hicho Mwajuma Hamza leo anawataka wajasirimali hao kuzingatia mafunzo yanayotolewa ili kujiongezea ujuzi wa kuendelea kutengeneza bidhaa zenye ubora unaohitaji katika soko huru la afirika kwani kunaushindani mkubwa na wajasiriamali wengine kutoka mataifa 55.

 

Amesema, kila mwaka wamekuwa wakiwafikia wajasiriamali wanawake zaidi ya milioni moja na kuwapatia elimu hiyo na lengo likiwa ni kuwainua kiuchumi kutokana na bidhaa wanazozalisha ziwe na ubora unaohitajika sokoni hivyo mafunzo haya yatakuwa njia ya mafanikio kwao kwani hata serikali imekuwa ikitengeneza mazingira wezeshi ya kibiashara.

 

“Niwaombe tuzingatie mafunzo kwa mada ambazo zinatolewa na wakufunzi wetu kutoka taasisi mbalimbali za serikali ikiwemo TBS na nyingine, tunataka kutengeneza wafanyabiashara wakubwa kutoka kwa wajasiriamli ambao watakwenda kushindana kwenye soko huru la afirika”Amesema Hamza.

 

Awali akifungua mafunzo haya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mboni Mhita amewataka kuzingatia mafunzo yatakayotolewa ili kuongeza ujuzi wa utengenezaji wa bidhaa, kwaniu kwenye uzalishaji wanawake wapo juu kulinganisha na kundi linguine isipokuwa wanakosa elimu ya kuzalisha bidhaa zenye ubora unaohitaka na hapo ndipo akibababa wanapowashinda.

 

Amesema,ili waweze kukua na kuwa wafanyabiashara wakubwa wajifunze kuchangamkia fursa za kibiashara zilizopo na kushindanisha bidhaa zao sokoni. Rais imekuwa akifungua fursa na milango ya kibiashara kwa makundi yote bila ubaguzi ili kumuinua mwanamke lakini wamekuwa waoga kujitokeza na inachukuliwa na akinababa pekee.