Amesema, hatua ya mikopo hiyo kutolewa na taasisi za kifedha imekuja baada ya kuwepo kwa malalamiko kwa baadhi ya wajasiriamali kutaka iwe inatolewa pia kwa mjasiriamali mmoja mmoja badala ya kwenye vikundi pekee na serikali imesikiliza ombi hilo na sasa inaweka utaratibu ziwe zinatolewa na taasisi za kifedha.
Mhita ameyabainisha haya leo wakati akifungua Mafunzo kwa wajasirimali kuhusu kanuni, taratibu na sheria za kufanya biashara kwenye soko huru la Afirika(AfCTA) yaliyoandaliwa na Chama cha wafanyabishara wanawake (TWCC) kwa ufadhiri wa Trade Maker kwa kushirikisha wajasiriamali zaidi ya 100 kutoka mkoani hapa.
Amesema, changamoto ya ukosefu wa mitaji ambayo ndio msingi wa kibaishara hivi karibuni inakwenda kutatuliwa na serikali yetu inayongozwa na Rais Samia Suruhu Hassani baada ya kusikiliza malalamiko na kuitolewa ufumbuzi hivyo mikopo ya asilimia 10 itakuwa ikitolewa na taasisi za kifedha ambazo zitaainishwa na serikali hapo baadae.
Nae Mkurugenzi wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake(TWCC) Mwajuma Hamza amesema,lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wajasiriamali wanawake waweze kukua kibiashara kwa kujua hatua sasa za utengenezaji wa bidhaa, kusajili na kupata masoko ndani na nje ya Tanzania.
Amesema, wanawake wamekuwa ndio wazalishaji wazuri wa bidhaa mbalimbali hapa nchini lakini wanakosa fursa za masoko ya uhakika kwasababu ya bidhaa zao kukosa ubora unaohitajika na ndio sababu ya kuwafikia na kuwaelimisha na mafunzo haya yatawajenga na kuwa na bidhaa zenye ubora mzuri.