Kilele cha onyesho hilo kilifanyika kwenye uwanja wa michezo wa 'Business' eneo la Buza kwa Mama Kibonge jijini Dar es Salaam juzi na kuhudhuriwa na wasanii mbalimbali wakiwamo wachanga.
Msanii huyo alipanda jukwaani akiwa na kundi lake la madansa sambamba na mdogo wake Abdul Kiba na kuimba baadhi ya nyimbo zake zikiwamo za 'Salute na Ndombolo ya Solo na kuibua shangwe za mashabiki.
Wakongwe wengine waliopanda jukwaani ni Chegge Chigunda kutoka TMK , huku akifuatiwa na mkongwe wa dansi Mwinjuma Muumin aliyetumbuiza kwa wimbo wake mpya wa 'Kwa Mpalange'.
Aidha, burudani nyingine zilizojiri ni pamoja na kinyang'anyiro cha kumpata Miss Buza ambapo taji lilikwenda kwa Amina Abdallah na pia wasanii mbalimbali wazawa wa eneo hilo la Buza walipata nafasi ya kutoa burudani.










