Waziri Bashungwa amechukua uamuzi huo baada ya wadau wa muziki ikiwemo mashabiki wa muziki huo na wasanii wenyewe kupinga vikali suala hilo wakidai haliwatendei haki wasanii.
Hatua hii inakuja zikiwa zimepita siku kadhaa tu tangu BASATA walipouzia wimbo wa msanii Ney wa Mitego unaojulikana ‘Mama’, kwa kumtaka abadili baadhi ya mashairi kwenye wimbo wake huo wa Mama, ambapo Ney mwenyewe alisema kwamba hayuko tayari kubadili chochote kwenye wimbo wake.










