Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, amesema hadi sasa tayari wamehojiwa watu watano kuhusiana na sakata hilo na sasa wapo nje kwa dhamana.
“Watuhumiwa hao ni Frida Kajala Masanja (36), Paula Paul Peter (18), Raymond Mwakyusa maarufu RayVanny (27), Claiton Revocuts maarufu Baba Levo (34), Catherine John na Juma haji (32).”
"Watuhumiwa hawa wote walikamatwa, wakahojiwa na kwa vile dhamana ipo wazi wapo nje kwa dhamana na taratibu za upelelezi zinaendelea zikikamilika jalada litaenda kwa Wakili Mkuu wa Serikali na kama akiona kuna jinai watafikishwa Mahakamani” amesema Mambosasa.










