Katikati ya wiki hii Simba iliandika ushindi wa nne mfululizo baada kuisigina Mgambo JKT mabao 5-1, huku Yanga ikichomoa dakika za mwisho na kufanya matokeo kuwa 2-2 walipocheza na Prisons ya Mbeya.
Ushindi huo uliifanya Simba kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo na kuishusha Azam FC. Simba ina pointi 39, moja nyuma ya Yanga.
Hata hivyo, pamoja na kudai kuwa wapinzani wao Yanga wawanaumia, Mayanja alikataa kuweka wazi kama kasi hiyo itawapa ubingwa.
Badala yake alisema kuwa ligi iko kwenye hatua ngumu na yenye ushindani mkubwa, hivyo hawezi kutabiri ubingwa.
"Muhimu ni kwamba tumeshinda mechi mfululizo, sitaki kuzungumzia nafasi ya Yanga ila nitafanya hivyo pale mchezo wetu utakapokaribia," alisema.
"Kwa sasa nafikiria mchezo unaofuata kabla ya kukutana na Yanga, lakini kazima nisema ukweli kwamba ligi bado ngumu."
Kuhusu ushindi wanaoendelea kuupata alisema: "Siri yake ni mazoezi mazuri ya kujenga na kuimarisha kikosi. Wachezaji kwa sasa wana moyo na ari ya ushindi kwa kila mchezo."
Aliongeza kuwa kila wanapomaliza mechi moja wanajipanga upya kwa ajili ya mchezo unaofuata.
"Kila mchezaji ni muhimu kwenye timu, leo (juzi) unasema Ndemla (Said) ameshuka kiwango, siyo sawa, mimi ninamtayarisha na ninampanga mchezaji kulingana na wakati, nani alijua kama Ugando (Haji) atacheza," aliongeza kocha huyo.
Ikiwa njiani kuelekea Shinyanga, jana kikosi cha Simba kilialikwa chakula cha mchana mkoani Dodoma na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ni mashabiki wa klabu hiyo wakiongozwa na Mussa Azzan 'Zungu' wa Jimbo la Ilala (CCM), Dar es Salaam.
Simba waanza kuichokonoa Yanga
05Feb 2016
Somoe Ng'itu
Nipashe
Simba waanza kuichokonoa Yanga
USHINDI mfululizo wanaopata Simba kwenye mechi za Ligi Kuu Bara umemtia jeuri Kocha Jackson Mayanja na tayari ameanza kuwachokonoa Yanga, akisema Wanajangwani hao wanapata maumivu makali kushuhudia pointi tatu-tatu zikiendelea kutililika Msimbazi.
Kocha wa Simba, Jackson Mayanja.










