Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli alisema mshindi wa kwanza katika mbio za Kilomita 42 kwa wanaume na wanawake atapata Sh. milioni 4 kila mmoja.
“Hii ndiyo zawadi kubwa kabisa kuwahi kutolewa kwa mbio zozote Tanzania na tunajivunia kuwa wadhamini wakuu wa mbio hizi ambazo zitafanyika Moshi Februari 28 mwaka huu,” alisema.
Alisema washindi wa pili watapata Sh. milioni 2, wa tatu Sh. milioni 1, wa nne Sh.900,000, wa tano Sh.600,000, wa sita Sh.400,000, wa saba Sh.350,000 wa tisa Sh.250,000 na wa kumi Sh.200,000.
“Ni matumaini yetu kuwa zawadi hizi zitawavutia watu wengi zaidi hasa Watanzania kushiriki na kushinda,” alisema na kuongeza kuwa zawadi zote kwa ujumla ni Sh.milioni 20.
Kwa upande wake, Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha, ambaye kampuni yake inadhamini mbio za Kilomita 21 alisema washindi wa kwanza kwa wanaume na wanawake watapata kila mmoja Sh. milioni 2, wa pili Sh. milioni 1, wa tatu Sh.650,000, wa nne Sh.500,000, wa tano Sh.400,000, wa sita Sh.325,000 wa saba Sh.250,000, wa nane Sh.150,000 wa tisa Sh.125,000 na wa kumi Sh.100,000.
“Tunajivunia kuwa wadhamini wa mbio hizi kwa mwaka wa pili mfululizo na ni matumaini yetu kuwa mbio hizi zitakuwa na mvuto mkubwa,” alisema huku akiwataka Watanzania wajitokeze kwa wingi kushiriki na kushinda.
GAPCO Tanzania nayo ilitangaza kuwa mshindi wa mbio zake za kilomita 10 kwa waendesha baiskeli za watu wenye ulemavu atapata Sh. milioni 1 kwa wanaume na wanawake, wa pili Sh. 400,000 wa tatu Sh. 300,000, wa nne Sh. 200,000 wa tano Sh.150,000, wa sita Sh.100,000 na watakaoshika nafasi ya saba, nane, tisa na kumi watapata Sh.75,000 kila mmoja.
Zawadi hizi zilitagazwa na Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi.
Kilimanjaro marathon zawadi usipime
05Feb 2016
Nipashe
Kilimanjaro marathon zawadi usipime
KILIMANJARO Premium Lager, wadhamini mkuu wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2016, wameendelea kuweka rekodi ya kutoa zawadi katika mbio zozote zinazofanyika nchini na kufanya mbio hizo kuwa za pekee na aina yake.










