Ushahidi upo mwaka 2002, alipotokea mnunuzi wa chai hiyo kulipa kiasi cha pesa za Kichina Yuan 180,000 ambayo ni sawa na Dola za Marekani 28,000 au Sh. miliioni 61.18.
Hiyo ni kwa chai hiyo yenye uzito wa gramu 20 tu ya chai hiyo ya Kichina inayoitwa Da Hong Pao.
Kwa ujumla katika utamaduni wa Kichina, suala la kunywa chai linapewa thamani kubwa tangu zama za miaka ya 1,500 iliyopita, jambo linalofanya wasiwe na utamaduni wa kuthamini mvinyo wa Kifaransa.
Hiyo ni kwa sababu chai yao imewajengea imani kwamba ina thamani kubwa, kuliko maono ya kwigineko, kwamba mvinyo wa Kifaransa ndiyo wenye thamani. Wachina wanauona ‘si lolote, si chochote.’
Inaelezwa kwamba, Dang Hong Pao, inayotokana na kuchumwa shambani, bei yake ni mara 30 ya dhahabu katika uzito huo huo.
Hivi sasa chai hiyo inauzwa kwa bei ya Dola za Marekani 1,400 au Sh. milioni tatu.
Aidha, kuna mtungi maalum wa chai unaouzwa kwa bei ya Dola za Marekani 10,000 ambayo ni sawa na Sh. milioni 21.85 na kuifanya kuwa miongini mwa chai zenye gharama kubwa duniani.
Nchini China, unywaji chai ni utamaduni unaopewa nafasi kubwa kama unavyoelezwa na Xiao Hui, mtengeneza chai mmoja wa mjini Wuyishan anayetamka:
“Inaonekana kumfaa kuanzia ombaomba, lakini zaidi kwa mtawala ambaye ana moyo wa Wabudha (waumini wa dini)”
Xiao na familia yake kwa kizazi na vizazi kadhaa, wameendelea na mazoea ya kwenda kwenye milimani iliko majani ya chai na kuomba Miungu ya Chai, waitwao Lu Yu, kuwaletea mimea.
Hivi sasa katika maduka mengi ya mjini Wuyishan, ambako kuna chai hiyo, huwa wana sherehe inayoigwa hata na Wajapani kuifurahia chai.
Hata hivyo, katika mji wa Wuyishan, chai ya Da Hong Pao inaelezwa walau ina bei nafuu.
Katika mji huo chai inauzwa kwa bei ya chini inayofikia Dola za Marekani 100 kwa kilo (Sh. 218,500).
Wuyishan ni mji uioko kando ya mto, Kusini mwa China. Xiao anongeza:”Da Hong Pao halisi ina bei kubwa zaidi kwa sababu.”
Lakini si Wachina walioipa thamani kubwa chai ya Da Hong Pao pekee. Huko nyuma mwaka 1849, mtaalamu wa mimea Mwingereza, Robert Fortune alifika katika milima ya Wuyishan kupanda mimea hiyo.
Hapo katika mika ya kati baada ya simulizi ndefu, chai hiyo ilitoweka, hadi ulipoingia utawala wa Rais Mao Tse Tung.
Mwaka 1958 walianza kujifunza tena kupanda mbegu za mimea hiyo na hadi kufikia mwaka 1990, mimea ya chai hiyo ilikuwa imeshamiri China.
Hivi sasa chai hiyo imemea katika sehemu nyingi za milima ya Fuji.
Namna ya uzalishaji wake hivi sasa, uko chini ya usimamizi wa kanisa na serikali ndiyo inafadhili mchakato mzima.
Uzalishaji wa chai hiyo ya thamani ni kidogo sana kwa mwaka. Miti hiyo ikiwa chini ya ulinzi mkali na miti hiyo inatofautiana kwa umri.
Baadhi ikiwa ni mipya na uvunaji hufanyika kila Mei Mosi, eneo hilo likizungushiwa kapeti nyekundu na mabinti warembo ndio wenye jukumu la kuvuna.










