Wajue ombaomba wa Marekani na staili yao ya kipekee

27May 2016
Salome Kitomari
Aliyekuwa Marekani
Nipashe
Wajue ombaomba wa Marekani na staili yao ya kipekee

YAPO mambo ambayo ukiyakuta katika zilizoendelea kama vile za Ulaya na Marekani, unaweza kushangaa, kwa kuwa yamezoeleka katika nchi za Afrika, Asia na kwingineko ambako kuna maendeleo bado ni duni.

Katika uwanja wa Ronald Reagan, Washington, National airport, kuna wazee ambao walikuwa wanatoa burudani kwa kucheza kwa umahiri mkubwa nyimbo za muziki ambazo ni za zamani.

Baadhi ya mambo hayo ni kuwapo ombaomba mitaani. Inaaminika katika nchi maskini, ndiko wanakopatikana.

Katika nchi za dunia ya kwanza kunajulikana kwa kuwa na mipango mizuri ya afya, elimu, maji, umeme na miondombinu muhimu ikiwa ni kuwawezesha wananchi wake.

Hiyo ni tofauti na nchi za dunia ya tatu, ambako matajiri wanaweza kupata mahitaji yote katika ubora unaotakiwa huku maskini wakishindwa kupata fedha za mlo wa siku.

Tofauti na Afrika ambako wazazi wa kike na kiume hukaa pembeni na kuwatuma watoto kuomba, Marekani wengi wanaoomba ni Waafrika, wazee na vijana wa Kizungu wengi ni walemavu wa kuona, huhakikisha staii yao ya kuomba ni kwamba ana kitu maalum cha kufanya.

USHUHUDA

Nikiwa nchini jijini Washington, Dc na baadaye Indianapolis, ambako kulikuwapo mikiki ya kampeni za uchaguzi zinazoendelea, muundo wa kuomba Marekani unatofautiana na wa nchini.

Uombaji wao ni wa kibunifu na ubunifu na jambo fulani la kuwafanya watu kusimama kwa ajili ya kusikiliza au kuona anachoonyesha.

Mathalan, mita chache kutoka Ikulu ya Marekani ambako watu wanaruhusiwa kupiga picha, kuna binti mwenye ulemavu wa kuona ambaye anaimba kwa sauti inayomgusa kila anayemsikiliza, huku akiwa na kapu la kukusanya fedha anazopewa.

Jijini Washington, DC kuna tofauti kubwa kati ya waombaji wa Wamarekani weupe na weusi.

Weupe huwa na kitu cha kuburudisha kama muziki au kupiga gitaa na kapu ili kujipatia fedha, wakiamini mtu hawezi kupata fedha bila ya kufanya kazi yoyote.

Kwa upande wa weusi, sikuona ubunifu, bali kuwapo kapu au kopo lililokuwa na jina lake na ujumbe wa kueleza kwanini anaomba, huku wengi wakijieleza wanatoka katika familia maskini au wana ulemavu, hivyo wanaomba wasamaria wema kusaidia.

Katika mitaa mbalimbali hasa maduka ya ‘super market’ (duka la kisasa) za kati kuna wanawake na vijana ambao huomba kwa kila anayeingia na kutoka katika mgahawa huku wakiomba kwa muundo wa kunyoosha mkono.

Mtanzania ambaye ni raia wa Marekani, ambaye hakutaka kutaja jina lake anaeleza ombaomba wengi hasa nyakati za usiku ni wanawake watu wazima, huku vijana wakizurura katika mitaa.

“Unawashangaa hao wenzako ndiyo wameshafika wako kazini na hapo hawaondoki wanaomba fedha na wakati mwingine wanatumika kingono.

“Hao ni wanawake ambao ni ‘single mother’ (wanawake wasio na waume) na wameshindwa kulea watoto ambao nao wapo mtaani kama hivyo,” anasema na kuongeza:

“Vijana unaowaona mtaani wana biashara nyingi ikiwamo madawa ya kulevya na wakidhulumiana ndiyo wanapigana risasi.

“Wanaweza kuiba gari la mtu kwa muda kwa ajili ya kutembelea na kulitekeleza…hii ni athari ya malezi ya upande mmoja kwa familia ambazo hazijiwezi.”

OMBAOMBA VIJANA

Nipashe ilishuhudia vijana wa umri wa kati ya miaka 20 hadi 30, wakiwa mtaani nyakati za usiku wakivuta sigara na wengine wakionekana katika ulevi wa dawa za kulevya, wakikimbia na kuongea kwa sauti nyakati za usiku.

Katika mji wa Indianapolis katika eneo la Art Garden Center kuna ombaomba wa kiafrika na kizungu, wakiwa na makapu yenye majina yao na historia yao kwa ufupi.

Wana tabia ya wanapopata fedha, huinia kwenye migahawa kwa ajili ya kununua chakula.

Katika mtaa mwingine karibu na Mnara maarufu wa Mashujaa wa Marekani wa jimbo la Indianapolis, alishuhudiwa binti anayetumia gitaa lake kuimba nyimbo mbalimbali, akiwa na kapu mbele yake.

Mtembea kwa miguu aliye mbali, anayesikia sauti nyororo ya binti huyo na anapokaribia, humkuta akaiwa na kapu mbele mbele yake kwa lengo la kujipatia fedha.

Kutokana na hali hiyo, wanaovutia kwa kuimba hupata fedha nyingi kutokana na wapita njia kutotaka kupita bila kutoa chochote.

Katika miji yote, kuna waombaji wanaoeleza historia zao, wazee wanaolala katika viti vya kupumzikia kutokana na kuchoka kwa hali ya uzee na kadhalika.

Mwenyeji wangu alinieleza kuwa wengi ni ambao maisha yamekuwa magumu kutokana na utaratibu wa nchi husika na wanajikuta hawana fedha za kugharamia maisha yao na wengine hawapendi kwenda kuishi katika kambi za wazee.

“Wengi wanaishi kwa huruma za wasamaria wema, kipindi cha baridi ya barafu hutafuta mahali pa kujificha baridi hasa katika maduka au migahawa mbalimbali kwani wapo ambao hulala katika vituo vya treni za umeme na mabasi.

Ni jambo linaloweza kuhisiwa la kusadikika, lakini ndiyo hali halisi iliyopo ikilinganishwa na Afrika.

Pia, si rahisi kuwakuta ombaomba katika taa za kuongoza magari kama ilivyozoeleka katika miji mikubwa ya Afrika Mashariki, ambako kwa kiasi kikubwa kunakabiliwa na foleni ya kupita kiasi.

VIWANJA VYA NDEGE

Katika staili nyingine, katika viwanja vya ndege kuna wazee wanaotoa burudani ya nyimbo za zamani, huku wakicheza kwa umahiri na kuna kapu la kuweka fedha mbele yao.

Katika viwanja wa Ronald Reagan, Washington na National Airport, nilishuhudia wazee waliokuwa wanatoa burudani za kucheza kwa umahiri mkubwa nyimbo za muziki ambazo ni za zamani nchini Marekani.

ULINGANISHI WA AFRIKA MASHARIKI

Mwaka 2014 nilitembelea Jiji la Kampala na wakati tukiwa kwenye foleni, watoto wakiwa na watoto mgongoni haijajulikana mara moja ni wao au wadogo zao, walionekana mitaani wakiomba, huku wazazi wao wakiwa pembeni na kuaminika inaaminika wanatumwa kufanya hivyo.

Katika mji wa Nairobi, Kenya nilitembelea mwaka 2014 nako kulikuwa na ombaomba wa watoto wenye watoto huku wazazi wao wakiwa pembeni na wamepachikwa jina la Chokoraa.

Jijini Dar es Salaam, kuna watoto wadogo wanaoomba, huku wazazi wao wakiwa kando. Waombaji hao huwa na watoto migongoni.

Pia, muundo mwingine unaotumika niwa katika viwanja vya ndege kuna wazee wanaotoa burudani ya nyimbo za zamani huku wakicheza kwa umahiri na kuna kapu la kuweka fedha.

Katika uwanja wa Ronald Reagan, Washington, National airport, kuna wazee ambao walikuwa wanatoa burudani kwa kucheza kwa umahiri mkubwa nyimbo za muziki ambazo ni za zamani.

Pia, muundo mwingine unaotumika niwa katika viwanja vya ndege kuna wazee wanaotoa burudani ya nyimbo za zamani huku wakicheza kwa umahiri na kuna kapu la kuweka fedha.

Katika uwanja wa Ronald Reagan, Washington, National airport, kuna wazee ambao walikuwa wanatoa burudani kwa kucheza kwa umahiri mkubwa nyimbo za muziki ambazo ni za zamani.

Jijini Dar es Salaam, kuna watoto wadogo wanaoomba, huku wazazi wao wakiwa kando. Waombaji hao huwa na watoto migongoni.