Uhaba huo si mara ya kwanza kuwapo nchini, kwani katika siku zilizopita, hali hiyo iliwahi kujitokeza na serikali kuingilia kutaka iingizwe kutoka nje.
Moja ya hatua zilizochukuliwa na serikali ni kufungua milango, sukari iingizwe kutoka nje ya nchi, kupunguza uhaba huo.
Ni kipindi kifupi kilichopita, hatua kama hiyo ilichukuliwa na baadaye baadhi ya wamilikli wa viwanda vya sukari, wakiwemo TPC ya Kilmanajaro walilalamika kwamba kuna sukari inayoingizwa nchini kimagendo na hazilipiwi kodi, jambo linaloathiri wazalishaji wa nchini.
Wakati bei elekezi iliyoko sokoni sasa ni Sh. 1,800 kwa kilo, katika uhalisia hakuna sukari yenye bei chini ya Sh. 2,400 huku kukiibuliwa kashfa kwa baadhi ya wafanyabiashara kuficha sukari.
Hadi sasa Tanzania ina viwanda vikuu vinne vya sukari ambavyo ni Mtibwa na Kilombero vilivyopo mkoani Morogoro, TPC ya Kilimanjaro na Kagera Sugar.
Vyote kwa pamoja vinazalisha wastani wa tani 350 za sukari, ikiwa ni pungufu kwa wastani wa tani 100 kutosheleza mahitaji halisi kitaifa.
Hiyo ndiyo hali inayotawala katika sehemu nyingi ukanda wa Afria Mashariki na Kati, mfano ukiwa nchini Kenya, takwimu za mwaka jana zinaonyesha kuna uhaba wa tani 200,000.
AFRIKA MASHARIKI
Kimsingi, ni vigumu kuepuka tafsiri ya mfumo wa uchumi Tanzania, ikiwamo uzalishaji wake, bila ya kuweka uhusiano wa karibu na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Wanachama wa EAC, jumuiya ambayo Tanzania ni miongoni mwa waasisi, pia inajumuisha Kenya, Uganda, Sudan Kusini, Rwanda na Burundi.
Katika Mtazamo mpana wa uhusiano na jumuiya hiyo, inafika mbali kwa mataifa kama Sudan, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Ethiopia na Eritrea, baadhi zikiwa wajumbe wa jumuia za maendeleo na uchumi za Comesa na SADC.
Taasisi ya kimataifa iitwayo BMI, mwaka jana ilifanya utafiti kutaka kupata uhalisia wa hali ya uzalishaji sukari katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Iliibuka na majibu kadhaa na ripoti yake ilikuwa na mtazamo we jumla unaotamkwa:“Licha ya ahadi kutoka mataifa ya Afrika Mashariki kuhusu kusaidia viwanda vyake vya sukari, hatuamini zao la sukari litaongezeka katika ukanda huo, kama ilivyotarajiwa itakuwa miaka michache ijayo.”
Kwa ujumla, sekta ya sukari katika ukanda wa Afrika Mashariki, inatajwa kuwa mwajiri mkubwa na mchangiaji mkubwa wa pato la taifa.
Nchini Kenya, kwa kurejea Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO), robo ya raia wake wanategemea sukari katika maisha yao kwa namna moja au nyingine, ikizingatiwa sehemu kubwa ya raia wanategemea kilimo.
Utafiti unanukuu Shirika la Maendeleo Maendeleo la Umoja wa Mataifa katika msimu wa mwaka 2014/15, Sudan ilishika nafasi ya juu kwa kuzalisha tani 780,000 inayoifanya ishike nafasi ya 25 kwa uzalishaji duniani.
Hiyo inaifanya taifa hilo kuwa na uzalishaji sukari wastani wa asilimia 220, kulinganisha na Tanzania inayoshika nafasi ya 45 kwa uzalishaji duniani.
Ethiopia nayo iko katika nafasi ya juu kuzalisha sukari ikiwa nafasi ya 27 duniani, ilhali Kenya iko nafasi ya 33 na Uganda ya 43.
Licha ya nafasi hizo kubwa za uzalishaji, bado mataifa hayo yanatofautiana katika kiwango cha matumizi na uhaba wa sukari kitaifa.
Mataifa wanachama wa jumuiya za EAC na Comesa, yamekubaliana na kupunguza vikwazo vya ushuru miongoni mwa wanachama wake.
Hata hivyo, kuna baadhi ya nchi zikiwamo Kenya na Tanzania, ambazo ni wanachama wa EAC, zimeweka zuio na vikwazo kadhaa kulinda soko lake la ndani la sukari.
MIPANGO YA UZALISHAJI
Nchi nyingi za Afrika Mashariki ziko katika mikakati ya kupanua uzalishaji sukari kitaifa.
Utafiti unaonyesha kuwa, uwezekano wa kuzalisha nishati ya umeme kutokana na miwa ni moja ya mambo yanayohamasisha uzalishaji zaidi wa sukari na nchini Ethiopia hiyo imeonyesha kuwa kivutio cha sukari zaidi kuzalishwa.
Nchi hiyo inaelezwa kuwa ina dalili ya kuwa kituo kikubwa cha kuzalisha sukari katika ukanda wa Afrika Mashariki na hata Afrika.
Mipango ya nchini hiyo ni kwamba, kupanua uzalishaji sukari kufikia tani 300,000 kabla ya mwaka 2020, jambo litakaloifanya kuwa mmoja wa vinara 20 duniani wa kuuza sukari nje ya nchi.
Moja ya dira ya nchi, kuweka sera na vikwazo vya kulinda uzalishaji wa ndani.
Wakati taifa hilo viwanda vyake vya kuzalisha sukari ni vya serikali, katika nchi kama Tanzania, Kenya na Uganda viwanda vilishabinafsishwa kwa zaidi ya miaka 20 sasa.
Inaelezwa kwamba, kushuka bei ya sukari katika nchi za Kenya na Tanzania kutachangia kuingeza uzalishaji kwa misingi, itazuia uingizwaji sukari ya nje na hivyo kuhamasisha uwekezaji wa ndani katika sekta ya sukari.
Uzalishaji sukari wa Kenya, unaelezwa kuathiriwa zaidi na kiasi kikubwa cha sukari kinachoingizwa kutoka nje, bila ya kutozwa ushuru mkubwa.
Ni mikkati ya kukabili upungufu wa ndani wa sukari na sera ya pamoja ya jumuiya ya uchumi ya Comesa, ambako Kenya ni mwanachama
VIKWAZO TANZANIA
Nchini Tanzania, miongoni mwa matatizo yanayotajwa katika ripoti ya utafiti wa uzalishaji sukari, ni pamoja na; Upungufu wa miwa, mfumo duni wa umwagiliaji mashamba ya miwa na barabara mbovu kuelekea mashambani na viwandani.
Katika Mpango wa Maendeleo ya Viwanda ya Miaka Mitano ya Tanzania iliyoisha mwaka jana, moja ya mikakati yake ni kuongeza uzalishaji wa sukari kitaifa.
Pia inaelezwa hali duni ya kifedha kwa wakulima wazalishaji wa miwa ya kuuzia viwanda vya sukari, inachangia kuwa na mashamba madogo kulinganisha na wenzao kwingineko.
Watafiti hao wa uzalishaji sukari katika Afrika Mashariki na Kati, wanaeleza kuwa hali mbaya iliyopo sasa Tanzania, ni zao la kilichoikumba nchi tangu mwaka 2010.
Katika ripoti yao, wanasema kushuka bei ya sukari kimataifa kuna mchango mkubwa kwa uzalishaji sukari nchini, na imekaribisha uingizwaji sukari kutoka nje, kinyume na sera za kiatifa.
Hiyo imekuwa na athari hata katika baadhi ya wazalishaji wakubwa wa sukari kupunguza kiwango cha bidhaa zao.
Ubashiri wa kitafita unaonyesha, huenda uzalishaji ukaendedlea kusuasua katika kiwango cha tani 350, wakati matumizi yatafika tani 600 ifikapo mwaka 2018/19. Ina maana kutakuweapo nakisi ya tani si chini ya 250.
Hiyo ina maana kwamba, juhudi za serikali kama zilizokuwa zikitangazwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ni muhimu katika kuongeza uzalishaji kupunguza nakisi ya kitaifa.
“Tunatarajia uzalishaji kuongezeka hadi tani 323,000 na kufikia kiwango kidogo itabaki kuwa kidogo kihistoria, kutokana na uzalishaji mkubwa katika nchi kama Brazil, Thailand na EU (JUmuiya ya Ulaya) tangu mwaka 2018.”
UGANDA NA SUDANI KUSINI
Utafiti unabashiri kwamba, katika miaka kadhaa ijayo, Uganda ambayo katika vipindi fulani hadi sasa ina mapungufu katika mahitaji yake ya sukari, katika miaka michache ijayo itakuwa inajitosheleza.
Kuna baadhi ya miaka ilifikia kuwa na ziada ya sukari, mfanio hao ni mwaka wa uzalishaji 2011/12 iikuwa na ziada,
huku mwaka wa uzalishaji 2014/15 imekuwa na upungufu.
Kutoka na mwelekeo huo, utafuti umebaini kwamba Uganda kupitia mwamvuli wa EAC inajaribu kusukuma majirani wake wa Kenya na Tanzania wafungue milango ya soko la sukari, ili iweze kuziuzia kila inapofaniki3ea kuzalisha ziada.
Uganda inang’ng’ania mwelekeo huo wa soko, ili kuvutia uwekezaji zaidi katika sekta ya sukari.
Sudani Kusini, taifa jipya ambalo pia ni mwanachama mpya wa EAC aliyejiunga mwaka huu, ina mipango ya kina kuzalisha sukar katika miaka michache ijayo, ikilenga kuzalisha tani milioni 10 hadi kufikia miaka mine ijayo – 2020.
Iwapo hilo litatimizwa na taifa hilo masikini ambalo linategemea zaidi uchumi wa kuzalisha mafuta, itakuwa mzalishaji mkubwa wa sukari katika ukanda wa Afrika Mashariki.
“Tunaamini kwamba, Sudani Kusini hadi kufikia mwisho wa muongo huu ambao utajitosheleza kwa sukari,” inafafanua ripoti ya utafiti.










