TUPIA MITO MIPYA
Njia rahisi na nyepesi kuliko zote ya kuzifanya kuwa bling’i ni kuweka mito mipya. Hii ina nguvu ya kubadilisha muonekano kwa njia zisizo na kikomo. Unaweza ukacheza na rangi, michoro, maumbo na hata malighafi iliyotengenezea foronya za mito.
Kama sofa unazotaka kufufua zina rangi nyeusi au isiyoegemea upande wowote rushia mito ya kuwaka kama vile rangi za chungwa, nyekundu au kijani cha ndimu au yenye doti doti za polka.
Kama sofa ni za maua tupia mito ya rangi moja na kama zina kitambaa cha ‘rafu’ tumia mito ya kitambaa laini. Mito ya sofa inakuja kwa kila staili kwa hivyo huwezi kukosa unayotaka.
KITAMBAA KIPYA
Vipo vitambaa vingi vya sofa vyenye maua, vya rangi moja au hata vya michoro mbalimbali ambavyo unaweza kumpelekea fundi akashonea upya kwenye sofa zako. Pia uzuri wa sofa nyingi za kisasa zina kava za kuvulika.
Fundi sofa Adam Kajembe, anasema ni eneo dogo sana kama vile zile sehemu za kuwekea mikono na mgongoni ambapo itamuhitaji fundi kushughulika nazo moja kwa moja kwenye na hasa kama sofa zenyewe ni za kutengeneza hapa hapa nchini una bahati maana itakuwa ni kazi rahisi zaidi.
BADILISHA MIGUU
Hii ni kweli! Unaweza kufufua muonekano wa sofa zako na kuzipa sura mpya kwa kubadilisha miguu yake. Uzuri wa sofa zinazotengenezwa zama hizi zimeunganishwa miguu tofauti na fremu za sofa yaani miguu sio muendelezo wa moja kwa moja kutoka eneo la kukalia.
Mara nyingi mgongo, kiti na eneo la kuweka mikono zimetengenezwa kama kitu kimoja na baadaye miguu inafungwa, anasema Kajembe. Kwa hivyo kama unataka kufanya mabadiliko ni rahisi sana. Aidha unaweza kufunga miguu mipya au kupulizia upya rangi miguu ya zamani na kuifunga tena na utashangaa tofauti utakayoona.
JAZA KUSHENI ZILIZOSINYAA
Kusheni hapa zinamaanisha ile mito inayokuja/inayotengenezwa na sofa ili kulikamilisha sehemu ya kukalia na ile ya kuegemea pamoja na kuegemeza mikono. Kusheni zinachukua nafasi kubwa zaidi kwenye muonekano wa sofa.
Mito hii ni muhimu na hatuwezi kuilinganisha na ile ya mapambo ya kutupia. Bila kusheni ni ngumu mgongo wa mkaaji kuwa na uwiano mzuri na sofa hilo. Kwa hiyo basi, kuendana na malighafi zilizojazwa ndani kutengeneza kusheni hizo, kuna wakati zinakuwa zimesinyaa.
Fundi Kajembo anashauri kutengeneza foronya mpya ya kitambaa kizito kama cha mablanketi na maduveti halafu uchukue malighafi iliyosinyaa kazi inakuwa rahisi kwa vile kusheni nyingi zina zipu, hivyo unafungua na kuongezea pamba au nyuzi za kujazia mito zinazopatikana madukani.
Baada ya hapo funga mto huo na uvalis he foronya ya nje na kuanzia hapo unakuwa na kusheni jipya ‘lililoshiba ‘lisilojasinyaa.
Sababu ya kutengenezea foronya za kitambaa kizito ni kuepuka mabondemabonde kwenye kusheni linaloboreshwa.
BADILISHA VITU
Japo njia hii si ya kugusa sofa moja kwa moja, ila kuna wakati unaweza kuitumia kuzingamsha zilizochoka , pale unaporesha vitu vinavyolizunguka. Jaribu kutundika picha mpya au hata kubandika karatasi za ukutani au ‘wallpaper’ nyuma ya ukuta ilipo sofa. Zikiwa zimezungukwa na vitu tofauti na vya kuvutia, sofa zinaweza kuvutia pia!
Zaidi tembelea www.vivimachange.blogspot.com Simu 0755 200023










