Khadijah Williams: Kutoka mtoto wa mtaani hadi Chuo Kikuu cha Harvard

10May 2016
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Khadijah Williams: Kutoka mtoto wa mtaani hadi Chuo Kikuu cha Harvard

KWA zaidi ya miaka 100, Taasisi ya Los Angeles 'Union Rescue Mission imekuwa kimbilio kwa familia zisizo na makazi.Nyakati za usiku,

khadija

wanawake na watoto hujazana ili kulala kwenye matandiko sakafuni katika makazi yao yaliyopo ghorofa ya nne,ambayo ni sehemu salama kwa wale ambao hawana makazi yao binafsi .

Khadijah Williams, mwanamke kijana kutoka California, alitumia muda mwingi wa usiku akifanya mazoezi yake katika moja ya vitanda hivi. Aliandika insha za Kiingereza,akafanya mazoezi ya hesabu na alisoma kwa ajili ya mitihani hadi taa zilipozika majira ya saa nne usiku
.

Khadijah alianza kuhama kutoka makazi moja hadi makazi mengine ya mama yake na dada mdogo alipokuwa na umri wa miaka sita. Wakati huo makazi yalikuwa hayapatikani, Khadijah anasema yeye na familia yake walikuwa wamelala katika vituo vya mabasi au mitaani.

Licha ya mazingira hayo, Khadija anasema mama yake daima alijitahidi kuwaongoza na dada yake ili wafikie kiwango cha juu. "Haijalisi tuliishi wapi , bila kujali jinsi hali zetu zilikuwa mbaya namna gani, mama yangu daima alikuwa na mtazamo chanya," anasema.

Katika miaka 12, Khadijah alihudhuria shule 12 tofauti, lakini aliendelea na rika lake huku akiutumia muda wake wa siku baada ya siku katika maktaba- Los Angeles Public Library. " Ilibadilisha maisha yangu," anasema.

"Maktaba ilinipa udhibiti wa baadhi ya nyanja za maisha yangu. Hata hivyo sikuweza kweli kudhibiti wapi napenda kuishi au kitu chochote, kudhibiti kiasi gani nilitaka kujifunza. "

Wakati wa kipindi cha masomo yake ya sekondari ya juu, Khadija aliamua kufanya chochote ambacho kingemfanya akae sehemu moja. Kutokana na hali hiyo, aliamka kila alfajiri saa 10:30 na kupanda basi kutoka Los Angeles 'Skid Row kwenda Jefferson High, ambayo ni umbali wa mwendo wa masaa mawili .

"Alitamani sana kuachana na aina hiyo ya maisha katika Skid Row au katika makazi kama hayo?" Anasema. "Hayo ndiyo yalikuwa malengo yangu ."

Khadijah kamwe hakuacha kuamini kuwa elimu ilikuwa tiketi yake ya kumfikisha kwenye furaha ya kudumu. Mwaka jana mwezi Mei alihitimu Jefferson High akiwa na tuzo ya juuya heshima. Sasa yupo katika Chuo Kikuu cha Harvard moja ya vyuo vya kifahari duniani ambacho watu wengi wanagependa kupata fursa ya kusoma hapo .

Licha ya kutoka makazi ya mitaani kwenye mazingira ya makahaba wa Skid Row, Khadijah anaikumbatia jamii yake mpya, Cambridge, Massachusetts. "Hali ni tofauti sana kutoka mazingira niliyozoea kuyatumikia (Katika) Skid Row, aina ya maisha ambayo unajisikia kukwama kwa sababu kila kitu kimechanganywa pamoja, "anasema. "Hapa, kila kitu kipo wazi. hewa ni safi...safi na ya wazi. "

Kama watoto wengine wanakulia katika mazingira hayo wanajua nini kipo juu ya vibanda huko nje na nini kilikuwa kinawezekana, Khadijah anasema mtazamo wao unaweza kubadilika.

"Kwa mtu yeyote, kutokuwa na makazi au vinginevyo, ambaye anahisi kama hayataki mazingira hayo na kudhani kuwa hawezi kufanya chochote kile ni kwamba wachukue mtazamo mpya kuwa wanaweza ," anasema. "Kwa wakati, ni kwamba hicho ndicho nimemudu kufanya hivyo.- Imani kwamba sababu wanaweza niliifanya.Unachotakiwa ni imani kwa sababu unaweza kufanya .Nimefanya ."