Namna ya kutambua kama unakunywa maji ya kutosha

10May 2016
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Namna ya kutambua kama unakunywa maji ya kutosha

Upungufu wa maji mwilini ni mbaya kwa mujibu wa utafiti mpya uliochapishwa katika jarida(Journal of the American College of Nutrition) la Chuo cha Marekani cha Lishe.

Watu wengi wanakabiliwa na wakati mgumu kutambua ni kiasi gani cha maji kinahitajika katika miili yao ili kuiwezesha ifanye kazi vizuri na kwa urahisi zaidi.

Watafiti wawili kutoka Chuo Kikuu cha New Hampshire wametengeneza mfumo rahisi wa kupima taratibu na kutoa mapendekezo ya namna bora ya kunywa maji kwa ajili ya kuzingatia afya ya mtu kwa mwili wenye siha njema.

Kiasi cha maji kinachohitajiwa mwilini na mtu ili kumfanya awe na uwiano sawa, kinategemea na mabadiliko ya mara kwa mara ya mwili katika hali ya joto na uzito, kiwango na muda wa mazoezi, ikiwamo chakula anachotumia kwa siku.

Mwili wa binadamu asilimia 66 ni maji, lakini unaweza kubadilika katika njia mbalimbali tofauti. Ni utata.Hata hivyo, watafiti wanadhani wamepata njia mbili ambazo zinaweza kutumiwa ili kuepuka kuwa na upungufu wa maji mwilini.

Katika utafiti huo, watafiti wamepata kipimo cha jumla cha maji yaliyomo katika mwili wa mtu , ambacho kinaweza kutofautiana kati ya mililita 600-900, na kujazwa katika mapengo ya maji ya ziada yanayohitajika mwilini.

Kisha walipima kipimo cha kiasi cha maji ya mtu binafsi anayotumia sio kutokana na maji tu, pia kutokana na kunywa vinywaji vingine na chakula; kisha, ni kiasi gani kinatolewa kwa njia ya kwenda haja ndogo na haja kubwa. Walibaini kuwa kiwango chote cha maji kinaweza kupimwa , kama maji, na kupotea kwa njia ya utoaji wa mabaki ya maji na vyakula mwilini

"Mahitaji ya maji yanatofautiana sana miongoni mwa watu kutokana na tofauti katika mambo yanayofanya mfumo wa utoaji wa maji mwilini na uwiano wake, hivyo, utoshelevu ni sambamba na namna maji yanavyoingia mwilini kwa kutumia njia ya kipimo cha tathmini," watafiti waliandika katika utafiti wao.

Kuweka mwili katika mizania ni muhimu kwa utaratibu maalum, kwa sababu watu wanaweza kupungukiwa na muafaka wa ulaji na maji. Jiulize wewe mwenyewe " Je ninakunywa maji ya kutosha?" Ni rahisi, gharama nafuu ya kutambua kama unywaji wa maji na utoaji wake kwa siku unakadiriwa kuwa kati ya 2.5 na 4 aunzi nane ya vikombe vya maji kila siku.

Kwa mujibu wa Mayo Clinic, upungufu wa maji mwilini unaweza kusababisha matatizo makubwa. Kama hunywi maji ya kutosha wakati unapofanya mazoezi, unaweza kuishia kutoa jasho jingi sana na kuchemka tumbo au uwezekano wa kutishia maisha ya kupatwa na kiharusi.

Uvimbe wa ubongo pia unaweza kutokea, ambao unaweza kuufanya mwili kuvuta maji sana tena ndani ya seli yako na kuvimba au kupasuka ubongo na hatimaye kuharibu seli.

Wengine ambao hawanywi maji ya kutosha wanaweza kupatwa na kifafa. Elektroliti, kama madini ya potassium na sodium, yanaweza kusaidia kubeba ishara za umeme kutoka kiini . Kutokana na upungufu wa maji mwilini, basi ishara zinaweza kusababisha misuli kukakamaa katika njia isiyo ya kawaida, kupoteza fahamu hata kuanguka kifafa.

Lakini moja ya madhara makubwa zaidi ya upungufu wa maji mwilini ni kuchangia kusababisha mshtuko, hata kuchochea shinikizo la damu kuchoka kabisa na kupungua kiasi cha oksijeni katika mwili. Figo kushindwa kufanya kazi, kukosa fahamu hata kusababisha kifo.Pia ni hatari zaidi kwa wale wanaokwenda bila maji kwa muda mrefu sana.

Upande mwingine, kuteketeza maji sana kunaweza kusababisha kifo chako. Figo hushindwa kudhibiti kiasi cha maji, chumvi, na maji mengine huchujwa na kutolewa mwilini. Maji ya ziada hutoka kwenye damu na kuingia kwenye seli ambazo huvimba kama puto na kusababisha madhara ya kiafya.

Wakati mtu anayekunywa maji sana katika kipindi cha muda mfupi, figo zao haziwezi kupata shida sana Inakuwa mapambano ya kuchuja damu na kusababisha damu kuwa na maji mengi na kutupa mbali kiasi cha chumvi.kwa njia ya maji ya ziada.

Kunywa maji kidogo sana ni hatari .Na kunywa maji mengi inaweza kukusaidia kudumisha maisha ya afya na kazi.