Kiba ambaye hajawahi kufanya kazi na watayarishaji hao alisema kuwa kwa sasa ni wakati wa kuwatafuta watu hao na kufanya nao kazi kwani anatamani jinsi wanavyomudu kazi hiyo.
"Kwanza kabisa niseme kuwa siku zote katika maisha yangu siwezi kumsahau mtayarishaji KGT ambaye amefanya kazi zangu kadhaa kutokana na darasa alilonipa kwenye muziki, lakini sasa ninatamani kufanya kazi na wakongwe hao," alisema Kiba.
Kiba pia aliwataka mashabiki wake kukaa mkao wa burudani, kwa madai kwamba kuna kazi kadhaa zinakuja, ambazo zitatayarishwa na waasisi hao kutoka MJ Records na Bongo.










