Hafisa Kazinja aibuka upya

01Mar 2016
Sabato Kasika
Nipashe
Hafisa Kazinja aibuka upya

HAFISA Kazinja alitarajia kuingia studio jana kutoa kitu kipya baada ya kukaa kimya kwa miaka miwili tangu alirekodi wimbo wa 'Mlala Nje'.

HAFISA Kazinja

Msanii huyo alisema jana kuwa hawezi kuweka wazi jina la wimbo wake mpya kwa sasa akihofia kuibiwa ubunifu.
"Ninajiandaa kwenda studio kurekodi wimbo wangu mpya, kwa sasa siwezi kuutaja kwa jina, huu utakuwa wa kwanza baada ya kimya cha muda mrefu," Kazinja alisema.

"Nakumbuka wimbo wa 'Presha' sikuupa jina kabla ya kurekodi, lilipatikana na baada kumaliza kurekodi, hata huu unaweza kubadilika jina ndiyo maana sioni sababu kulitaja kwa sasa.'

Kazinja ni miongoni mwa wasanii waliowahi kutamba katika muziki wa kizazi kipya na nyimbo zake nyingi amekuwa akitumia mtindo wa 'zuku' ambao umechangia kumpaisha matawi ya juu.