Wachezaji ni kama wamechanganyikiwa, hawajui nini kinaendelea kuhusiana na hatima ya Kocha Louis van Gaal.
Stori zimekuwa nyingi kuhusua hatima ya VCan Gaal, ambaye hata yeye hajaelezwa lolote kuhusiana na nini kitafuata.
Wakati wachezaji wakiendelea kubaki njia panda bila kujua hatima ya kocha wao, uvumi kuhusu Jose Mourinho kutua Old Trafford unazidi kuongezeka.
Wachezaji wakongwe kwenye klabu hiyo inayozidi kupoteza mwelekeo kwenye mashindano, nao pia hawafahamu lolote kuhusu kocha wao wala ujio wa Mourinho kama inavyodaiwa.
Kushindwa kujua nini kinaendelea ndani ya klabu hiyo, ndiyo sababu kubwa ya maisha kuwa magumu kwenye vyumba vya kubadilisha nguo.
Habari kutoka ndani ya klabu hiyo, zinadai wachezaji wamepoteza hamasa na ari ya kushindana kutoka na kutumia muda mwingi kujadili hatima ya kocha.










