Kocha huyo raia na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa, alichukua mikoba ya kuinoa timu hiyo kutoka kwa Rafael Benitez aliyetimuliwa Uwanja wa Bernabeu Januari mwaka huu.
Tangu alichukua mikoba na kuwa kocha kamili, Zidane alianza vizuri kabla ya juzi kufungwa nyumbani bao 1-0 na wapinzani wao wakubwa wa mji wa Madrid, Atletico Madrid katika mechi ya Ligi Kuu Hispania.
Matokeo hayo yameifanya Los Blancos kuwa nyuma kwa pointi nane kutoka kwa vinara wanaoongoza Ligi, Barcelona.
Sasa Zidane anadai kuwa, mwaka ujao kutakuwa na mabadiliko makubwa kwenye klabu hiyo.
"Mwaka unaofuata kutakuwa na mabadiliko makubwa ya kocha na wachezaji. Lakini kwa sasa lazima mambo yasonge mbele kwa vile kuna kitu tunahitaji," alisema Zidane.
Real Madrid, pia imetupwa nje ya michuano ya Kombe la Copa del Rey mwanzoni mwa mwaka huu. Pia haijawahi kutwaa taji la La Liga tangu ilipofanya hivyo mara ya mwisho mwaka 2012.









