Nay amesema anaona kauli hiyo haina maana kwa kuwa mtoto ni wake na kuongeza kuwa hawezi kubishana na Ommy sababu hana mtoto hata wa kusingiziwa.
“Mimi kwenye wimbo ‘Shika Adabu Yako’ nilimchana Ommy, kiukweli tetesi zilizopo mtaani kuwa jamaa kwa kuwa hajawahi kuonekana na mwanamke hapa Bongo,” amesema Nay.
Amedai kuwa Ommy, anaishia tu kuposti picha za wanawake waliopo Ulaya wakimbusumbusu, na kuhoji kwa nini hamuoni na wanawake wa nchini.
Ameongeza kuwa wanawake wa Kiafrika ndio wazuri zaidi na wana kila kitu na kusisitiza kuwa kuhusu mtoto hawezi kubishana naye kwani hana mtoto na akipata mtoto atamjibu kuhusu DNA.










