Akizungumza jana jijini, kiongozi wa bendi hiyo, Mule Mule, alisema kuwa maandalizi ya utambulisho wa BMM yamekamilika na watatumia siku hiyo kukitambulisha kibao chao kipya kiitwacho 'Watabiri'.
Mule Mule ambaye amejiunga na bendi hiyo akitokea FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma' alisema kuwa wasanii mbalimbali watasindikiza uzinduzi wa bendi hiyo na kuwataja baadhi yao kuwa ni Mrisho Mpoto, Barnaba na mshindi wa BSS mwaka jana, Kayumba.
Alisema kwamba bendi hiyo imejipanga kuleta mapinduzi ya muziki wa dansi Tanzania na kurudisha heshima ya muziki huo kama zilivyokuwa zikitamba Msondo Ngoma na Sikinde.
Mmiliki wa bendi hiyo, Deus Macha alisema amejiandaa kuwekeza kuinua wasanii chipukizi na kwa muda huu hatajali kiasi cha fedha atakachotumia.










