Mafunzo hayo yanatarajiwa kuhusicha makocha makocha 40 na yana lengo la kuwaongezea ujuzi walimu hao ili kwenda sambamba na sheria za mchezo huo zilizobadilika.
Katibu wa Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA), Ramadhani Namkoveka, alisema mafunzo hayo yatashirikisha makocha kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini na wa kuanzia ngazi ya awali na yatafanyika kwenye Ukumbi wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika iliyopo jijini Dar es Salaam.
Namkoveka alisema mafunzo hayo yataendeshwa kwa muda wa wiki moja na chama kilitoa nafasi kwa makocha kutoka mikoa yote ya Tanzania kushiriki.
Aliwaomba makocha wote waliothibitisha kushiriki kwenye mafunzo hayo kufika mapema ili darasa lianze kama ilivyopangwa.










