Man United kucheza na timu ya mashoga

15Feb 2016
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Man United kucheza na timu ya mashoga

MANCHESTER United wamekubali kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya mashoga, Stonewall FC ya England.
Mechi hiyo ni maalumu kwa ajili kuadhimisha miaka 25 ya mfuko wa Stonewall ambao ndio unaomiliki timu hiyo.

WACHEZAJI WA MANCHESTER UNITED

Hata hivyo, katika taarifa yake Manchester imesema itachezesha wachezaji veterani na siyo wanaotumika kwenye mechi za Ligi Kuu.

"Kama ambavyo wengine wamesema kwamba siyo vizuri kwa sisi kucheza mechi hii," alisema Mkurugenzi Richard Arnold.
"Hata hivyo, tu tumeamua kucheza mechi hii kwa kuwatumia wachezaji wakongwe na baadhi ya wachezaji wa timu ya wafanyakazi."

United itatumia pia mechi hiyo kuonyesha mshikamano na mfumo LGBT unaoendesha timu hiyo kabla ya kuivaa Arsenal kwenye Uwanja wa Old Trafford, Februari 28.