Morocco alisema hayo juzi baada ya mechi hiyo kumalizika kwenye Uwanja wa Amaan na kutaja sababu nyingine ya kupoteza mchezo huo ni wachezaji wake kukosa uzoefu wa mechi za kimataifa.
Kocha huyo msaidizi wa timu ya Taifa (Taifa Stars), alisema pia kutowafahamu wapinzani wao kulichangia kupotea na kuruhusu mashambulizi ya mara kwa mara kwenye lango lao.
"Tumefungwa na timu bora ukilinganisha na sisi, pia tulikuwa hatuwafahamu, ndio maana kipindi cha kwanza tulizidiwa lakini kipindi cha pili baada ya kujua aina ya mchezo wao, tulibadilika na kuonyesha uhai kiasi fulani," Morocco alisema.
Kutokana na kichapo hicho, Maafande wamejiweka kwenye mazingira magumu kusonga mbele, kwani sasa watahitaji kushinda angalau mabao 4-0 katika mchezo wa marudiano utakaofanyika baada ya wiki mbili.










