Tanzania nayo imeanza kuathiriwa na vitendo hivyo kwa baadhi ya watu kujibadilisha wajihi wao kwa kutumia madawa makali kama vile Lotion zenye viambata vikali au vidonge maalum.
Baadhi ya wasanii bongo fleva, Bongo movie na vijana wa kiume wamejikuta wakijiingiza katima matumizi ya vipodozi vikali kwa ajili ya kuondoa rangi zao za asili ‘nyeusi’ na kuutaka weupe.
Hata hivyo wataalam wa masuala ya urembo wanasema matumizi makubwa ya vipodozi vyenye viambata vikali vina madhara kwa binadamu.
Wanasema pamoja na kumpa mtu urembo wa muda mfupi, maisha yake yapo hatarini kutokana na seli za mwili kuharibiwa.
ATHARI
Athari za moja kwa moja zinazoonekana ni mtumiaji kupata magonjwa ya ngozi, saratani, ngozi kusinyaa na kubabuka na kuweka alama nyeusi mwilini.
Kwa wale wanaoutumia vidonge kujibadilisha rangi ya mwili, wapo hatarini kuwa wagumba na magonjwa mengine yaliyotajwa.
USHAURI
Watalaam hao wanashauri watu kujikubali rangi zao na kuona wapo sahihi kuwa hivyo walivyo.
Wasifikirie umaarufu au utanashati unatokana na mabadiliko ya muonekano wa viungo, badala yake wazingatie na matumizi ya lugha nzuri.










