DCEA yateketeza ekari 50 ya bangi Arumeru

07Mar 2024
Zanura Mollel
Arusha
Nipashe
DCEA yateketeza ekari 50 ya bangi Arumeru

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini wameteketeza zaidi ya ekari 50 za bangi katika kijiji cha Kisimiri Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.

Mkuu wa Operesheni Kanda hiyo(DCEA) Innocent Masangula amesema wananchi hao wamebadili njia ya kilimo hicho kwa kufanya kilimo mseto cha mazao mbalimbali(nafaka) pamoja na zao haramu la bangi.

 

"Zao hili haramu lilikua limelimwa kwa kuchanganywa na mazao ya chakula kama vile Mahindi, Maharage na alizeti, hata hivyo kwa makadirio ni zaidi ya gunia 350 za bangi zimeteketezwa" amesema Masangula.

 

Afisa Elimu Jamii( DCEA )Kanda ya Kaskazini Shabani Miraji ametoa wito kwa wananchi kujiepusha na kilimo haramu cha dawa za kulevya ikiwemo bangi ambayo inatajwa kuhatarisha usalama wa mazao ya chakula.

 

"Adhabu inayotolewa kwa mujibu wa sheria ya kudhibiti na Kupambana na dawa za kulevya Na 5,ya Mwaka 1

2015 inasema kwa wanaojihusisha na biashara hiyo na ulimaji wa mazao haramu ikiwemo Bangi kifungo ni cha miaka 30 au maisha jela" amesema Benson Mwaitenda Ofisa Sheria (DCEA).