Kiwanda hicho kinatarajia kufunguliwa hivi karibuni na kitakuwa na mitambo ya kisasa zaidi na kimejengwa kando ya soko la madini la Mkoa wa kimadini Kahama, hivyo wanunuzi na wachimbaji wanawajibu wa kusafisha dhahabu yao kabla ya kupeleka kwenye masoko ya kimataifa.
Profesa Kikula ameyabainisha haya wakati alipofanya ziara yake ya kukagua ujenzi wa jengo hilo na soko kuu la madini mkoa wa kimadini kahama, ambapo amesema uwekezaji wa namna hii unafaaa kuigwa na wawekezaji wengingine kwani inasaidia pia kudhibiti utoroshaji wa madini hayo.
Pia amesema, utoroshaji bado upo ila kwa kiasi kulinganisha na miaka ya nyuma na hii ni kwasababu ya uwepo ushirikiano baina ya wachimbaji wadogo, polisi jamiii pamoja na tume ya madini hivyo na kupongeza kampuni ya SAB GOLD LTD kwa uwekezaji ambao utasaidia kuwepo kwa ushindani sokoni na serikali kupata mapato yake.
Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Abdulrahiman Sangey, amesema, dhahabu nyingi zinazopokelewa sokoni zitakuwa na asilimia 70 hivyo wao watazisafisha hadi kufikia asilimia 99 kabla ya kuingizwa na kuuzwa sokoni.
Hata hivyo amesema,moja ya faida ya kiwanda hicho kitachaji malipo ya serikali na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa wastani asilimia 7.3 kulinganisha na wale wataouza dhahabu zao kwenye masoko ambapo wanachajiwa asilimia 9.3 hivyo sasa watakuwa na changua la wapi wanatakiwa kwenda kusafisha na kuuza dhahabu zao.