Watakao sherehekea mwaka mpya kwa pikipiki kuchukuliwa hatua

28Dec 2023
Shaban Njia
KAHAMA
Nipashe
Watakao sherehekea mwaka mpya kwa pikipiki kuchukuliwa hatua

MKUU wa Kitengo cha Usalama Barabarani mkoani Shinyanga, Wensesilaus Gumha, amewataka waendeshaji wa vyombo vya moto hasa pikipiki na bajaji kuacha tabia ya kusherehekea kuingia kwa mwaka mpya kwa kutumia vyombo hivyo kwani wamekuwa wakisababisha kutokea kwa ajari na watu kupoteza maisha.

Amesema, sherehe za kuupokea mwaka mpya wa 2024 ni vema wakasherehekea wakiwa katika vyumba za ibada wakimuomba Mungu au majumbani mwao nasio kuendesha pikikipiki na bajaji kwa fujo au kuchoma mataili na watakaobainika watakuchukulia hatua za kisheria kwa sababu siku hiyo askari watakuwa barabarani.

Gumha ameyabainisha hayo leo wakati akizungumza na madereva wa pikipiki na bajaji katika viwanja vya Shirika la Nyumba Halmashauri ya Manispaa ya Kahama na kuwambusha kuzingatia sharia na kuheshimu alama za usalama barabarani wawapo barabara wakisafirisha abiria ili kuepuka ajali zisizokuwa na ulazima.

Amesema, siku ya kushereheka mwaka mpya na wakibaini unasherehea mwaka kwa kutumia pikipiki kwa kuendesha kwa fujo kukatiza mitaani, ukipata ajari watajua alikuwa mhuni kwani anayesoma udereva na kujitambua hawezi kuyafanya hayo kwasababu atakuwa anajua sharia na anahatarisha usalama wake na wengine.

Mwenyekiti wa Waendesha pikipiki mkoa wa Shinyanga Idisamu Mapande amekili kuwepo kwa uvunjifu wa sharia za usalama barabarani kwa madereva wake na wakati mwingine kwa makusudi na niwale ambao ni wageni kwani kazi yao hiyo inaajili vijana kila siku hivyo wataendelea kuwaelimisha kwa kuwapatia elimu.

Balozi wa usalama barabarani Godfrey Allex amesema, amekuwa akishirikiana na jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani katika kutoa taarifa pale anapoona sharia zinavunjwa na wengi wamekuwa wakichukuliwa hatua na kuwataka madereva kuzingatia sharia kwani wanapata ajari na kupoteza maisha na kuacha wake wajane na watoto yatima.