Kinana ameyasema hayo leo, Desemba 24, 2023, jijini Arusha, alipokuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa 10 wa Jukwa la Vijana wa Kiislamu Mkoa wa Arusha (JUVIKIBA).
Kinana amesema kuwa, endapo taasisi za kijamii zitajikita kuhamasisha elimu ya ufundi, wengi wao watapata utaalamu katika fani mbalimbali ambazo zitawawezesha kujiajiri, kuajiri wenzao na hata kuwa na sifa ya kuajiriwa katika maeneo mengine ya fani walizozisomea na kujifunza.
“Niwapongeza vijana kwa kujitoa kupambania elimu ya ujasiriamali na ufundi, pia ninaamini jitihada hizozitawalipa matunda mema kwa kujiingizia kipato badala ya kusubiri ajira kutoka serikalini,” amesema.









