Meneja uhusiano wa bendi hiyo, Ramadhan Pesambili aliiambia Nipashe kuwa rapa huyo atatambulishwa kwenye ziara ya bendi itakayofanyika mikoa ya Kanda ya Ziwa Victoria.
Pesambili alisema kuwa Akudo Impact inatarajia kuanza ziara hiyo ambayo ni rasmi kwa ajili ya kuendesha kampeni ya kupinga mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino).
Itaanza wiki chache zijazo. "Tutaongozana na Totoo katika ziara hiyo kwa sababu ni mwanamuziki wetu ambaye alirudi kundini hivi karibuni, hivyo tutafanya utambulisho wake huko," alisema Pesambili.
Pesambili alisema mbali na Totoo Ze Bingwa, bendi hiyo imemnasa mnenguaji nyota Sabrina Mathew aliyewahi kufanya kazi katika bendi ya African Star 'Twanga Pepeta'.










