Walter ambaye ni mshindi wa Bongo Star Search mwaka 2012, amesema kwa muda mrefu sasa hajaonana na Nay wa Mitego kutokana na kwamba harakati zao zipo tofauti kwani yeye sasa anaimba injili, lakini anamkubali kwa ngoma zake, na hata maneno ambayo aliwahi kumwambia kipindi fulani yalimuongezea umakini kwenye muziki na maisha kwa ujumla.
Nay alishawahi kumchana Walter miaka ya nyuma, kitu ambacho wengi walitarajia kuwa wanaweza kuwa hawana uhusiano mzuri.
"Na siyo Nay tu, marafiki wangu wengi sana sijaonana nao kwa sababu wao wapo kwenye bongo fleva na mimi injili, hatuonani, kama tumetofautiana harakati fulani kwa hiyo si rahisi kukaa pamoja. Unaona leo umeniuliza, ilinibusti, ilinifanya nifahamike zaidi na hata kama kuna sehemu nilikosea ilinifanya nijitafakari," alisema.









