Pamoja na kukemewa, lakini kuna baadhi ya wanaojihusisha kufanya vitendo hivyo, huamua kujitangaza kupitia mitandano ya kijamii na wengine kujionyesha waziwazi.
Inasikitisha kuona vijana wanaotegemewa kuwa viongozi wa baadaye kujiingiza katika janga hilo ambalo hata kwenye vitabu vitakatifu limekemewa.
Hivi sasa kwenye mikutano ya siasa, kwenye nyumba za ibada, mikutano ya shule, suala kubwa linalojadiliwa ni vitendo hivyo viovu vilivyoshamiri nchini.
Badala ya Taifa kuzingatia mambo muhimu ya maendeleo, inabidi ichukue sehemu ya muda kuzungumzia vitendo hivyo ambavyo vinaharibu tunu ya nchi.
Viongozi wa kisiasa na dini wote sasa wameweka nguvu zao kukemea suala hilo ili vijana wa Kitanzania wasiendelee kuangamia.
Kama vitendo hivyo vikiachwa viendelee kushamiri basi hapo baadaye kutakuwa na taifa la hovyo na hata ile dhana ya vitabu vitakatifu vya kuwataka wanadamu wakazaane haitakuwa imetimizwa.
Inasikitisha kuona vijana wa kiume wenye nguvu eti wanatembea barabarani wakiwa wamelegeza mikono na macho.
Hii dhambi aliyeileta nchini anastahili adhabu kubwa, kama sio duniani basi ahera kwa kusababisha ukiukwaji wa uumbaji wa Mungu.
Sasa hivi ukienda maeneo ya ufukweni unaweza kutoa machozi, kwa sababu utashangaa wanaume wanavyokumbatiana ni kama mtu na mke wake au mchumba wake.
Wengi wa vijana wanaharibikiwa kwa sababu ya tamaa ya kuwa na vitu anavyomuona navyo rafiki yake, bila kujua kuwa mwenzake amevipata kwa kufanya kazi kwa bidii.
Akiona kijana mwenzake anaendesha gari zuri au ana nyumba nzuri na ana pesa ya kumwezesha kuishi bila tatizo, na yeye anataka kumuiga kwa kutafuta njia ya mkato.
Ndiyo maana hata kwenye vitabu vitakatifu kuna zile amri kuu kumi na moja wapo inakataza kutamani kitu chochote alichonacho mwenzako.
Amri zile zinatoa mafundisho makubwa na kama waumini wangeyazingatia, haya yanayotokea sasa yasingekuwapo.
Vita hii ina hitaji nguvu ya pamoja kuanzia kwa wazazi nyumbani, jamii inayowazunguka, viongozi wa dini na kimila pamoja na serikali ili kuhakikisha vitendo hivi vinakomeshwa kabisa nchini.
Watoto wanaharibika wakiwa bado wadogo na baadhi yao wazazi wao wanakuja kugundua tayari wakiwa wamekwisha haribika.
Kinachouma zaidi ni kuona baadhi ya watoto hao wanaharibiwa na ndugu wa karibu wanaoaminiwa na wazazi.
Kuna jamii ambayo hata ikiona vitendo hivyo vinatendeka wananyamaza kwa kuogopa kuonekana wabaya. Lakini wakumbuke kuwa leo wanapoona watoto wa wenzao wanaharibiwa, kesho watakuwa wa kwao na watakuja kujuta kwa kutotoa ushirikiano kwa wenzao.
Pia, kuna watu wanaoaminiwa kuwa watoto wakipelekwa kwao watakuwa salama, wamekuwa ndio chanzo cha kuharibu watoto hao.
Imekuwa ngumu sasa kuamini hata ndugu wa karibu kuwa na mtoto wako na ile heshima na kumpa mgeni kulala na watoto chumba kimoja imeanza kuondoka kwa kuogopa vitendo hivyo kufanyika.
Vitisho vya watenda makosa hayo, vinasababisha watoto kuogopa kusema ukweli kwa wazazi wao na kubaki wakiharibiwa.
Nguvu ya ziada inahitajika kukomesha vitendo hivi visiendelee kutendeka na kuharibu nguvu kazi ya taifa.










