Bosi COSTECH: Miaka miwili kiserikali, tunaneemeka kwa teknolojia

31Mar 2023
Renatha Msungu
DODOMA
Nipashe
Bosi COSTECH: Miaka miwili kiserikali, tunaneemeka kwa teknolojia
  • uchumi *Yabeba tenda kuhudumia nchi kiufundi

HADI sasa serikali iliyo madarakani ikiwa na miaka miwili inaendelea kutumia nyenzo zake za maendeleo, ikiwamo elimu. Hapo Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), iliyoanzishwa kisheria mwaka 1986, nayo inanyoosha mikono imebeba haki ya jukumu kuu la kuwa Mshauri Mkuu wake katika Sayansi,

Ndani yake inasema, sasa inatumia huduma zake kiuchumi kunufaisha nchi katika mahitaji yanayoangukia mahitaji yao kiuchumi.

Hadi sasa, inawajibika kisayansi kwa maendeleo ya teknolojia nchini kupitia Mfuko wa Taifa wa Uendelezaji Sayansi na Teknolojia (MTUSATE), ikitoa ruzuku kugharamia utafiti, teknolojia na ubunifu nchini.

Chanzo kikuu cha fedha za mfuko serikalini zinatumika kujenga, kukarabati na kununua miundombinu na vifaa vya maabara, katika taasisi za utafiti na maendeleo, ili kuwapatia ruzuku wabunifu wa maeneo mbalimbali nchini.

Hapo inajumuisha kugharamia miradi ya utafiti, uwezeshaji, uhalalishaji teknolojia na kusambaza matokeo ya utafiti na ubunifu, pia ajira.

Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dk. Amos Nungu, anaiambia Nipashe kuna mafanikio katika kipindi cha mwaka 2021 hadi 2023, serikali kuongeza pato la serikali kupitia MTUSATE, kutoka Sh. bilioni 3.5 mwaka 2020/21 hadi Sh. bilioni 4.4 mwaka 2021/22.

Dk. Nungu anataja mafanikio mengine, ni miongozo sita ya kuendeleza utafiti na ubunifu nchini, inayoandaliwa na kuanza kutekelezwa, pia kwa wadau maendeleo.

Anasema fedha za MTUSATE zimeongezeka, ikilinganishwa na mwaka 2021, kutumikia katika mambo mbalimbali.

Pia, anataja matumizi ya kuchangia uendeshaji Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) nchi nzima na kuendeleza wabunifu uliopatikana kupitia mafunzo ya ubunifu, ushauri, kuwaunganisha na taasisi kisekta, kulingana na mahitaji yao ya ruzuku.

Hapo anatoa mfano, mshiriki wa MAKISATU 2020 mwenye ubunifu wa Mita za Kulipia maji kabla ya matumizi amewezeshwa kuunda kampuni changa.

Anasema kampuni tanzu chini ya COSTECH, imeingia makubaliano na Mamlaka ya Maji Vijijini (RUWASA) mwaka 2021/22 kuwa mteja mkuu, ikipewa fursa kufunga mita hizo mikoa yote 25 ya Tanzania Bara. Hadi sasa imeshafunga mita 20 katika mikoa; Tanga, Pwani, Morogoro, Iringa na Njombe.

Dk. Nungu anafafanua, ni fedha zimefadhili miradi 10 ya utafiti kwa Sh. 2,281,119,320; mitatu ya miundombinu ya utafiti, ikiwamo katika maeneo ya afya (tiba asili), mifugo na uvuvi katika Taasisi ya Chanjo Kibaha (TVI – Kibaha), Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) na Taasisi ya Tiba Asilia (ITM) iliyopo katika Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili, yenye jumla ya gharama ya 1,188,397,320/-

Pia, kuna miradi mitatu ya kitafiti katika maeneo ya kilimo na Uvuvi kwa taasisi ya TARI-Mikocheni, UDSM na SUA iliyogharimu kiasi cha Sh. 360,000,000.

Pia, kunatajwa miradi minne ya utafiti katika maeneo ya kilimo na viwanda kwa taasisi za vyuo vikuu kadhaa, zikigharimu Sh. 732,722,000.

UTAFITI WABORESHWA

Dk. Nungu anasema, COSTECH imeratibu na kuzindua miongozo sita ya utafiti, katika kusudi  la kuendeleza ubora wa viwango vya utafiti nchini.

Inadhamiriwa kwa miaka mitano ijayo, 2021/22 hadi 2025/26, tume inawezesha taasisi nane zenye mamlaka za kusimamia tafiti kisekta, nne Bara na nne visiwani.

WASHIRIKA WA MAENDELEO

D. Nungu anaitaja COSTECH ni mwanachama wa asasi Global Research Council (GRC), ambayo ni sehemu ya mataifa 11 kutoka mabara manne; Afrika, Ulaya, Asia na Amerika Kusini duniani.

"Mchakato wa kuwapata washindi unaendelea na kuongeza watafiti sasa wamekaribishwa kwa hatua ya kuandaa maandiko yao," anasema Dk. Nungu.

Anafafanua, nia ni kujengwa uwezo na ujuzi kwa watafiti, kujenga mtandao, pia kuongeza maarifa kwa watafiti, ili kuwezesha kuwapo tafiti zenye tija kwa matokeo chanya kwa jamii.

Anaeleza, COSTECH imeshafahamika kimataifa kwa tija na inaomba kuwa mdau katika kundi la wataalamu wanaojadili usawa katika ubia wa ngazi ya wafadhili.

Lingine linatajwa ni COSTECH kushiriki katika mradi wa kukuza ubunifu kusini mwa Afrika, ambayo ni ushirikiano kati ya serikali ya Finland na nchi tano za Afrika; Tanzania, Msumbiji, Namibia, Botswana na Afrika Kusini.

Hapo Tanzania ilishafanikiwa kupata Sh. bilioni 2.030 (Euros 720,000) kwa miradi mitano iliyotekelezwa nchini.

Pia inatajwa kuna Sh. milioni 100 kwa Watanzania walioshiriki miradi ya SADC, ikijivunia ni kwamba kupitia mradi wa KItanzania, kumepelekwa ubunifu wa ubinfu kwa taasisi kama; Chuo Kikuu cha Nelson Mandela, nchini Zambia.

Hapo kwa miradi ya ubunifu, COSTECH imekuwa sehemu ya timu iliyopata miradi miwili kutoka Umoja wa Ulaya kupitia Atamizi yake (DTBI) na Ukumbi Bunifu (BUNI):

 

COSTECH kupitia kampuni tanzu DTBI, inashiriki katika mradi uitwao Hubiquitous, unaolenga kuanzisha na kukuza ushirikiano baina ya bara la Afrika na Ulaya, kwenye ubunifu wa kidigitali unaoshirikisha kampuni changa za teknolojia ya digitali, kutoka nchi tano za Afrika na nne Ulaya.

Barani Afrika, nchi zinazoshiriki ni Tanzania, Kenya, Ghana, Misri na Nigeria, kila moja ikiratibu ushiriki wa kumbi bunifu tano kwenye nchi husika.

Dk. Nungu anasema Tanzania imeratibu upatikanaji na ushiriki kwenye mradi 10,  ikwamo kupitia taasisi; SIDO Tech hub (Arusha), SUZA Tech Hub (Zanzibar) , Bonge Tech (Dar es Salaam), Capita space (Dodoma) na Buni Hub (Dar es Salaam), akinena ni jambo la kujivunia.

Hadi sasa Tanzania imeshaandaa kitabu kinachoelezea mfumo wa ubunifu barani Afrika, ili kuimarisha uhusiano wa kampuni changa zilipo Afrika na Ulaya, kwenye teknolojia ya kidigitali.

Dk. Nungu anafafanua, COSTECH kupitia ukumbi wake wa ubunifu (BUNI Hub) inashiriki katika mradi wa AfriconEu, lengo ni kuunganisha kumbi za ubunifu kutoka bara la Afrika na za bara la Ulaya.

Anasema jumla ya kumbi za ubunifu 11 zinashiriki kutoka Afrika; Tanzania, Uganda, Ghana na Nigeria na nchi za Ulaya ni; Uingereza, Ugiriki Italia, Ureno na Slovenia.

Pia, anasema, wanaendelea na mazungumzo na Shirika la Maendeleo la Sweden (Sida), lifadhili utafiti kwa miaka mitano, wakiwa wametenga Sh. bilioni 10.

KUHUSU MRADI WA HEET

Inaelezwa pia, COSTECH inanufaika na uwekezaji uliofanywa na serikali ya awamu iliyopo, kupitia mradi wa Mageuzi ya Elimu na Uchumi wa Juu, wastani wa Sh. bilioni 18.4

 

 

Top of Form

Bottom of Form

Bottom of Form