Utata uliojivika katika siasa ya uchumi kati ya Russia na Ulaya

22Mar 2023
Na Mwandishi Wetu
URUSI
Nipashe
Utata uliojivika katika siasa ya uchumi kati ya Russia na Ulaya
  • • Kiulizo; nani anawajibikia uhaba chakula ?

HADI sasa Umoja wa Ulaya unaendelea na kampeni yake kusambaza habari, ikielekeza lawama Russia, katika zama iliyopo mwaka mmoja wa vita kati yake na Ukraine, kwamba inasababisha uhaba wa chakula na hasa kwa nchi maskini duniani.

Hilo linatokea sambamba na kupatikana ufafanuzi kwamba, inatoa mchango mkubwa katika kuvuka kikwazo cha uhaba wa chakula uliopo duniani.

Lakini ikivaliwa miwani, ukweli unaoashiria ni kwa EU inatumia tatizo la upatikanaji chakula duniani, kutimiza malengo binafsi ya kisiasa, pasipo kutathmini matokeo hasi yanayoweza kuathiri mataifa yanayoendelea, hasa barani Afrika.

Kuna mifano ya hivi karibuni kutoka kwenye mkutano wa Halmashauri ya Kilimo na Uvuvi ya Umoja wa Ulaya uliofanyika Januari 30 mwaka huu, nchi kama Austria, Ubelgiji, Croatia, Cyprus, Jamhuri ya Czech, Ugiriki, Hungary, Latvia, Malta, Poland, Romania na Slovenia, ziliwasilisha taarifa isiyo rasmi.

Ni taarifa iliyopewa jina “Kuhakikisha uthabiti na uwezo wa ushindani wa kimataifa wa Umoja wa Ulaya: haja ya msaada wa dharura na msimamo wa kimkakati wa kuendesha biashara ya kilimo”.

Kimsingi, ni aina ya waraka unaoeleza sababu ya wakulima katika Umoja wa Ulaya kwa jumla, kushinikizwa kwa njia zisizo na mifano.

Bila shaka sasa kuna tathmini kutoka Umoja wa Ulaya, inayotamka “matatizo ya leo yanasababishwa na uvamizi haramu wa nchi ya Russia.”

 

MZIZI WA MKASA

Sababu halisi zinazounda hali ya sasa zinapaswa kuanikwa na vigezo kadhaa vinavyobeba ukweli kama; mlipuko ugonjwa UVIKO-19; mfumuko wa bei mkubwa, kuongezeka bei za rasilimali za nishati, nikiamini hazihusiki kabisa au moja kwa moja na kinachoitwa “uvamizi haramu wa nchi ya Russia.”

Pia, ni ngumu kusahaulika maendeleo makubwa yanayohusu kujengwa uchumi wa kijani na kidigitali, hali kadhalika ushindani wa kimataifa.

Ni sababu zilizoongeza thamani ya uzalishaji na kusambaza mazao ya kilimo. Kwa kifupi, hali ngumu ya sasa, ni matokeo ya mambo kadhaa ikiwamo siasa ya Umoja wa Ulaya wenyewe.

Inapozungumziwa uhaba wa nishati, jamii inapaswa kutilia maanani hali ya uhaba wa nishati ulioanzia Marekani kuuagiza Umoja wa Ulaya usitishe matumizi ya nishati kutoka Russia na badala yake, ununue gesi bei ya juu zaidi Marekani.

Uhalisia unaotawala, umoja huo una mikabala miwili tofauti ya kutatua matatizo ya kilimo nchini kwao na katika nchi nyinginezo.

Kwa upande mmoja, EU inatamani kuchambua sababu halisi za matatizo hayo, ili kupata uamuzi sahihi. Lakini, kwa upande mwingine zinaangukia kujengwa sura ya kushitakiwa Russia kulingana na hali inayoendelea katika siasa yake na Ukraine.

Pia, ni wakati EU inaendelea kulazimisha nchi nyingine duniani zifuate siasa yao, ambayo imeshaleta matokeo ya kutia shaka kwa uimara wa sekta kilimo duniani.

Bei kubwa za mbolea na vyakula au tatizo la kugawa chakula, mara zote si kitu kingine, yasipokuwa matokeo ya moja kwa moja ya vikwazo haramu dhidi ya nchi ya Russia vinavyozuia usafirishaji mbolea na kudhoofisha masoko ya nishati.

Licha ya miito mingi ikiwamo kutoka EU na jumuiya nyingine za dunia, umoja huo haukufanya  chochote kuboresha hali ya leo, huku ukiendelea kutangaza vikwazo vingi dhidi ya Russia.

 

MIKAKATI TATA

Wenyeji wa Ulaya wanapendelea kuzungumzia fidia za pesa kwa wakulima wao na njia za kuhakikisha uwezo wa ushindani wa EU kwenye masoko ya kimataifa.

Jambo la kuvutia ni kwamba, nchi zilizoshiriki katika mkutano wa Halmashauri ya EU ya Kilimo na Uvuvi ya Januari 30, mwaka huu zimeendana na mawazo ya Rais Vladimir Putin.

Hapo inaunda ujumbe kwamba kukosekana chakula ni matokeo ya moja kwa moja ya vikwazo dhidi ya Russia na siasa zinazoendeshwa na nchi tajiri zaidi duniani, kununua chakula kwa fedha taslimu, pia kwenye siasa  ya vizuizi nishati.

Ni hali inayojionyesha kwenye waraka unaoitwa: “Matatizo yanayohusika na ongezeko la uingizaji wa bidhaa za kilimo kutoka nchi ya Ukraine”.

Ni waraka uliowasilishwa na ujumbe wa Poland kwa niaba ya nchi kama Bulgaria, Jamhuri ya Czech, Hungary, Poland, Romania, Slovakia kwenye mkutano huo huo wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya ya Kilimo na Uvuvi uliofanyika mnamo Januari 30 mwaka huu.

Waraka huo unaendana na pendekezo liitwalo “solidarity lanes initiative” lililolenga kuwezesha usafirishaji bidhaa za kilimo hasa mazao ya nafaka kutoka nchi jirani za Umoja wa Ulaya, kwenda nchi nyingine zinazokabiliwa na ukosefu wa chakula.

Iko wazi kwamba, waraka unafichua hatua zilizochukuliwa mwezi Juni mwaka jana, kuwezesha uingizaji bidhaa kutoka Ukraine kwenda Ulaya, ikiwamo kuondolewa kwa mwaka mmoja ushuru wa forodha wa bidhaa zinazotoka Ukraine, ili kuchangia kuongezeka chakula.

Kinachopelekwa kutoka Ukraine kwenda Ulaya, kinajumuisha mazao ya nafaka, sukari, nyama ya ndege wa kufugwa, unga na vyakula kadhaa vinavyotengenezwa kwa maziwa, asali, juisi ya tufaha, mbegu za alizeti na mizabibu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa katika nchi wanachama wa EU, uingizaji ngano kutoka Ukraine uliongezeka maradufu kati ya mwaka 2021 na sasa hali inaonekana ngumu, hata nchi za Ulaya zilizotajwa mapema.

Leo likofika, zinatoa madai ya kutia saini waraka maalum, bidhaa za kilimo zitokazo Ukraine kupitia EU kufikia masoko yanayolengwa, kupita masoko ya nje ya umoja huo, jambo linalotajwa linaweza kuleta vurugu katika masoko hayo na ndani ya Ulaya.

Maudhui ya nyaraka hizo, yanatambulisha kwamba: Kwanza, kinyume cha matangazo bora kuhusu upatikanaji chakula katika nchi maskini nchi za Ulaya zinanunua kwa kasi bidhaa za kilimo kutoka nchi ya Ukraine, ili kujihifadhi na kuhakikisha ustawi wao.

Pili, inaelezwa kwamba nchi za Umoja wa Ulaya zikisafirisha vyakula katika nchi maskini zenye mahitaji makubwa na zinazitumia nchi maskini kama mahali daraja na kujinufaisha kwenye sekta ya kilimo.

Kwa mujibu wa gazeti moja la Austria (jina tunalo) ni kwamba nafaka kutoka Ukraine ilisafirishwa katika nchi za Uhispania, yanayotumika kuwa malisho kwa nguruwe.

Sababu ya kufanyika hivyo, ni majibu kwamba Uhispania, iliipatia Ukraine pendekezo la kibiashara bora, hivyo ikaijibu kwa kuipatia nafaka kwenda Hispania.