Ni zama ambazo Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, anatimza mwaka mmoja na miezi minne kazini, akiendesha mageuzi na mikakati yake kuiendeleza nchi.
Ripoti ya Mwaka ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu, ni waraka wa jitihada za serikali kutetea hali ya binadamu, utawala wa sheria na usalama wa taifa.
Hapo inamaanisha, bado serikali nchini haijakidhi vigezo vyote vya kutokomeza usafirishaji haramu wa binadamu, lakini imefanya jitihada kubwa kudhibiti.
“Marekani imepokea kwa furaha hatua kubwa iliyopigwa na serikali ya Tanzania katika kukabiliana na usafirishaji haramu wa binadamu, ikilinganishwa na hali ilivyokuwa katika vipindi vilivyotolewa taarifa hapo awali,” anatamka Balozi wa Marekani nchini, Donald Wright.
Anaendelea: “Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam unaipongeza serikali ya Tanzania, Sekretarieti ya Kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu.”
Pia, anaelekeza pongezi kwa vyombo vya usimamizi wa sheria, Idara ya Ustawi wa Jamii, taasisi katika sekta ya sheria, mashirika yasiyo ya kiserikali na wabia wengine kwa mafanikio hayo, kukabili usafirishaji haramu wa binadamu.
Ripoti ya mwaka jana, imetaja hatua zilizopigwa na serikali nchini, inayojumuisha kufanyika uchunguzi wa kesi za usafirishaji haramu wa binadamu, kuwabaini waathiriwa wengi wa biashara hiyo na uratibu mzuri kitaifa na kimataifa, kuimarisha mafunzo kwa maofisa serikalini.
Hapo kunatajwa serikali ilipitisha Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu wa 2021 hadi 2024 na kufanywa marekebisho makubwa katika Sheria ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu Mwaka 2008.
Ni jitihada zinazotajwa kufanywa kwa ushirikiano na asasi za kiraia, wanasheria wasio na mipaka na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu.
Hapo kunaelezwa, ni kati ya serikali na asasi za kiraia katika utekelezaji shughuli za kujenga uelewa, kwa lengo la kuzuia usafirishaji haramu na kuwasaidia waathiriwa wa biashara hiyo.
“Tunaihimiza serikali ya Tanzania kupanua zaidi kazi nzuri iliyofanyika katika kipindi cha mwaka uliopita,” anashauri Balozi Wright.
SURA YA MAPAMBANO
Ni wiki iliyopita, kinamama nchini wamesherehekea siku yao, huku bado wapo baadhi yao ambao wameshuhudia au wanashuhudia madhila ya aina fulani.
Hilo ni zao la ama kujua au kutokujua, kwamba sehemu ya magumu hayo huchangiwa na ndugu, pia watu waliokosa uadilifu.
Dunia ikisherehekea Siku ya Wanawake Duniani, nchini Tanzania bado wengi wanakumbwa na madhila ya usafirishaji haramu binadamu kuvuka mipaka, vilevile ndani yake ikibeba jina la ‘Utumwa Mambo Leo.’Akizungumza na Nipashe, Ofisa Mwandamizi wa Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi(ATS), Alexander Lupilya, anakitatafsiri ’ni kitendo cha kumsafirisha mtu, kumtumikisha kikazi pasipo malipo.’
Anaorodhesha mikoa iliyoathirika zaidi nchini ni Simiyu,Mwanza, Shinyanga, Geita, Dodoma, Singida na Dar es Salaam, hasa nyanja ya usafirishaji haramu wa binadamu nchini.
Kwa mujibu wa ofisa huyo, wanawake wengi wanasafirishwa kwa ajili ya kutumikishwa kikazi, pia ngono. Ni katika kundi la watu 150 waliookolewa kwenye matukio ya utumikishwaji, asilimia 72 na asilimia 28 iliyobaki ni watu wazima, hasa wanaopelekwa nchi za uarabuni kufanya kazi za ndani.
Inaelezwa, wapo wanawake huwekwa katika kumbi za starehe maarufu Kasino au madanguro, kutumikishwa kingono na kuna wakati, hukutana na magumu wanapokataa kuendana na ajira hiyo.
Pia anataja, saluni za kiume zinaonekana kuwa kificho cha wanawake baada ya kunyolewa wateja wa kiume. Wao huwafanyia usafi wateja na kisha kuwauliza kama wanahitaji huduma ya kingono.
Inatajwa, kuwapo baa, wanawake hawalipwi, bali wana namna ya kupata chao, ikioanishwa na ngono. Ndio kunatajawa kujitokeza kwenye migawaha na nyumba za kufanya masaji, kuna wanawake wasioajiriwa.
HATUA ZA KISERIKALI
Ofisa Lupilya anasema, kati ya Julai mwaka jana na mwezi uliopita, kuna kesi 13 za usafirishaji haramu wa binadamu zimepelekwa mahakamani katika mikoa mbalimbali nchini, zikiwa katika hatua mbalimbali.
Anaeleza hadi sasa, wameshawaokoa jumla ya wahanga 150 wa usafirishwaji haramu wa binadamu, waliokuwa wakitumikishwa kinguvu.
Lupilya anaainisha mchanganuo wake; kwamba 118 ni wanawake na 42 wanaume, kati yao 98 ni watoto wenye umri chini ya miaka 18, hivyo anasema ni wazi kinamama ni waathirika wakubwa wa usafirishaji huo.
Kwa mujibu wa ofisa huyo, sehemu kubwa ya matatizo wanayokumbana nayo wahanga, ni kufanyishwa kazi bila malipo, vipigo, kunyimwa chakula, kukosa haki ya matibabu wanapoumwa, kufanyishwa kazi wakiwa wagonjwa na kufungiwa ndani wasikutane na wengine.
Vilevile anataja madhila ya kulishwa makombo na hawana muda wa kupumzika wanapofanyishwa kazi za ziada, wanalala katika mazingira magumu, mfano jikoni na stoo.
Hapo Lupilya anafafanua kwamba, Sheria ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu ya Mwaka 2008, ilikuwa ikitoa adahabu au kulipa faini, hivyo wasafirishaji wengi waliokuwa wakikamatwa walichagua kulipa faini, hata wakaachiwa huru.
Anasema, baada ya kuonekana tatizo linazidi kuongezeka, mwaka 2022 kikao cha Bunge kilifanya mabadiliko ya sheria hiyo, ikiongeza adhabu kuanzia kifungo cha miaka mitano na zaidi hadi maisha, huku faini yake ikiwa kati ya Sh. milioni tano hadi Sh.milioni 350.
Pia, ofisa huyo anaeleza kwamba imebainika kufanyika biashara hiyo, ina ukaribu wa umasikini na hali ngumu ya maisha, hivyo anatoa rai umma, kuchangamkia mbadala wa kimaisha unaojitokeza, ikiwamo serikalini .
SHIRIKA LA WAHAMIAJI
Shirika la Wahamaji Duniani (IOM), linaeleza tafiti zilizofanywa na UNODC zimeonyesha kushuka usafirishaji haramu wa binadamu baada ya kuripotiwa mlipuko wa COVID-19
Inasema ni kipindi jamii nyingi zilikuwa karantini na wanawake wakaonekana kusafirishwa nje ya nchi kutumikishwa kingono, kwa mtindo wanapofika, hati zao za safari huzuiliwa na wenyeji wao.
"Ukishakua huna hati ya safari katika nchi ya watu unaanza kuingia matatizoni ,wengi wanaosafirishwa hurubuniwa kwa kuelezwa kupata maisha mazuri" linafafanua shirika hilo.
KWANINI BIASHARA HARAMU?
Sababu kubwa inatajwa ni kukua soko la ngono duniani, pia hitaji la wafanyakazi wa bei rahisi katika viwanda na mashamba makubwa duniani, hali kadhalika kuwapo ushindani kati ya masikini na tajiri katika kukidhi matakwa yao.
Ofisa Uhusiano wa makao makuu ya Jeshi la Uhamiaji Tanzania, Mrakibu Msaidizi Azizi Kirondomara, anakiri usafirishaji haramu wa binadamu ndani na nje ya nchi, upo nchini ikiwamo kwa mabinti wanaosafirishwa kufanya kazi za ndani mijini, bila kulipwa stahiki, au kutolipwa kabisa na wananyanyaswa.
" Huchukuliwa kutoka mikoa ya lringa asilimia 15; Kilimanjaro asilimia tisa na Morogoro asilimia tisa. Walichukuliwa kwenda kunyonywa katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na visiwani Zanzibar.
“Hata hivyo, aina kubwa ya unyonyaji ilikuwa ni utumikishwaji kazi za ndani asilimia 55 na…(biashara ngono ) asilimia saba,” anaeleza.