Mabondia kutoka mikoa mbalimbali wanaendelea kuchuana katika Mashindano ya Taifa kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, Dar es Salaam na tayari yameingia hatua ya robo fainali.
Hadi sasa hakuna bondia hata mmoja aliyefuzu kushiriki michezo ya Olimpiki hiyo.
Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga alisema mabondia 80 wameingia hatua hiyo ya robo fainali na mchujo wa kwanza utahusisha mabondia 20.
"Leo (jana) tumeingia hatua ya robo fainali, kesho watakaoingia nusu fainali watakuwa wamejulikana na mabondia watakaochaguliwa kwenye timu ya Taifa watakuwa 20," alisema Mashaga.
Alisema timu hiyo itaingia kambini kwa ajili ya kujiandaa kuelekea Cameroon watakapokwenda kupambana kuanzia Machi 9 hadi 20 itasiwamiwa na Kocha Mkuu, Remmy Ngabo.










